BEKI
wa kushoto wa klabu ya Liverpool, Aly Cissokho anatambua kuwa sio aina
ya mchezaji ambaye ni maarufu lakini ameapa kucheza kwa bidii wakati
akiwa Anfield. Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa, amekuwa sehemu ya
kikosi cha kwanza cha Liverpool toka uanze mwaka huu lakini amekuwa
akishambuliwa na baadhi wachambuzi wa mambo ya soka akiwemo Michael Owen
kwa jinsi anavyomiliki mpira na anavyoshambulia.
Na wakati akikiri kuwa hawezi
kumridhisha kila mtu, amepania kuonyesha thamani yake mpaka mwishoni mwa
msimu wakati uamuzi utakapotolewa kama anaweza kupata mkataba wa kudumu
kutoka Valencia. Cissokho amesema malengo yake ni kujituma kadri
anavyoweza kwa ajili ya Liverpool na kufurahia kila dakika halafu
itajulikana huko mbele itakavyokuwa. Beki huyo alicheza mechi yake ya
kwanza toka achukuliwe kwa mkopo kutoka Valencia Agosti 24 katika mchezo
wa ligi dhidi ya Aston Villa lakini siku tatu baadae alipata majeruhi
yaliyomfanya akae nje ya uwanja kwa wiki sita.Cissokho akionesha kiwango moja ya mechi Liverpool walipocheza na Newcastle.Aly Cissokho, Daniel Sturridge (katikati) waLiverpool wakipongezana pamoja na Luis Suarez
No comments:
Post a Comment