RAPA mpya wa Extra Bongo Grayson Semsekwa na mnenguaji Asha Sharapova walikonga nyoyo za mamia ya mashabiki wa
muziki wa dansi waliojitokeza katika onyesho maalum la utambulisho wa
wanamuziki hao lililofanyika katika Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar es Salaam.
Semsekwa na Sharapova walitangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita kujiunga
na Extra Bongo wakitokea bendi hasimu ya African Stars Twanga Pepeta tayari
kujiandaa na uzinduzi wa albamu mpya ya bendi hiyo inaoitwa Mjini Mipango
itakayozinduliwa Februari 22 mwaka huu katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala.
Mara baada ya Mkurugenzi wa bendi hiyo Ally Choki kumpandisha jukwaani rapa
huyo na kuanza kuimba vipande vya rapu zake za kwenye nyimbo za zamani kama
Regina Zanzibar, Double Double, 3x3 mashabiki walijikuta wakishindwa kutulia kwenye
viti na kwenda kumtunza hali iliyofanya ukumbi kuchangamka kwa mayowe ya
furaha.
Kwa upande wake Sharapova alionyesha umahiri wa kunengua sambamba na
wenzake katika shoo maalumu ya kinadada ambapo licha kutofanya nao mazoezi
aliweza kuendana na staili za mtindo mpya wa bendi hiyo 'Kimbembe'.
Wanamuziki hao wanaonguna na wenzao tayari kuingia kambini wiki hii
kujiwinda na uzinduzi wa albamu ya 'Mtenda Akitendewa' unaosuburiwa kwa hamu na
mashabiki wa muziki wa dansi.
Mtenda Akitendewa ni albamu ya nne kwa bendi hiyo iliyoasisiwa kwa mara
kwanza mwaka 2003 ikiwa na waimbaji Ally Choki, Bashiri Uhadi, Bob Kissa,
Richard Maarifa, Khalidi Chokoraa, Flora Moses, rapa Greyson Semsekwa.
Wengine ni Bonzo Kwembe anapiga Solo, Efraim Joshua,George Gama wanapiga
besi, Rythm na Thabit Abdul anayepiga kinanda na Imma Chokolate anayepiga ngoma.
Albamu ya kwanza iliitwa '3x3' ambao ni wimbo uliokuwa kwenye albamu
nyimbo nyingine ni 'Regina Zanzibar', 'Tuchunge Wazazi au Fikiri Madinda',
'Nunu Milenium' 'Walimwengu Remix' na 'Odise'.
Albamu ya pili ilitwa 'Bullet Proof' ikiwa na nyimbo kama 'Double Double'
na 'Regina Zanzibar' kabla ya kusambaratika mwaka 2004 na bendi hiyo kuanzishwa
tena mwaka 2009 na kuibuka na 'Mjini Mipango
No comments:
Post a Comment