CHAMA cha
Ngumi za Ridhaa mkoa wa Dar es Salaam kimemteua aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya
ndondi ya taifa Remmy Ngabo kuwa, Mkurugenzi wa Ufundi na Maendeleo ya
Wachezaji.
Shirikisho
la Ndondi Tanzania BFT hivi karibuni lilimtema Ngabo mwenye cheti cha daraja la
kwanza cha ufundishaji ndondi pamoja na makocha wengine kuifundisha timu hiyo
na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Selemani.
Akizungumza jijini
Mwenyekiti wa DABA Akaroly Godfrey alisema kuwa wamemteua Ngabo kuwa mkurugenzi
wa ufundi ili awasaidie katika kuuendeleza mchezo huo hapa Dar es Salaam.
Awali,
ilidaiwa kuwa, Ngabo aliingia matatani na uongozi wa BFT baada kocha huyo
kuudhuria Uchaguzi Mkuu wa chama cha mkoa wa Dar es Salaam, ambao BFT walidai
kutoutambua na baadae kushiriki katika mashindano yaliyoandaliwa na mkoa huo.
Mashindano
hayo ya wazi ya mkoa wa Dar es Salaam yalifana huku yake ya taifa ya wazi
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Packers kutokuwa na msisimko baada
ya baadhi ya mabondia nyota kutoshiriki mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment