UEFA imemfungulia Mashitaka Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini kwa matamshi yake mara baada ya Timu yake kufungwa 2-0 na FC Barcelona Jumanne iliyopita Uwanja wa Etihad kwenye Mechi ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI.Pellegrini alimponda vikali Refa kutoka Sweden, Eriksson, na kudai Refa huyo hakuwa na msimamo wa kutopendelea Timu moja.Jana Pellegrini aliomba radhi kwa kubatuka baada ya Mechi lakini hilo halikumsaidia kwani UEFA imemfungulia Mashitaka na shauri lake litasikilizwa na Bodi ya Nidhamu ya UEFA hapo Februari 28.
Patashika kwenye lango la Barca!
Barca walifunga Bao la Pili katika Dakika ya 88 kupitia Dani Alves na Timu hizi zitarudiana huko Nou Camp hapo Machi 12. Akiongea na Wanahabari baada ya Mechi hiyo, Pellegrini alisema: “Nina malamiko, si Penati tu na Kadi Nyekundu. Katika Mechi nzima hatukuwa na Refa aliechezesha Mechi sawa kwa pande zote!”
Aliongeza: “Aliamua Gemu. Aliamua Mechi kwa sababu ilikuwa faulo ya Sergio Busquets kwa Navas. Refa alikuwa Mita 3 tu na hakupiga filimbi na baada ya hapo ile faulo ya Demichelis ilikuwa nje ya Boksi, hivyo si Penati. Makosa makubwa kwa Timu kama Barca yanafanya iwe ngumu kushinda!”
Pellegrini alienda mbali zaidi na kudai kuwa Refa Jonas Eriksson hakupaswa kupewa Mechi hiyo na UEFA kwa sababu alishawahi kukwaruzana na Barcelona Mwaka 2012 kwa kuwanyima Penati kadhaa walipocheza na AC Milan huko San Siro na kutoka 0-0 kwenye Raundi ya Mtoano ya UCL.
Mwaka huo, Kocha wa Barca wakati huo, Pep Guardiola hakulalamika chochote, lakini Magazeti ya Spain yalikerwa sana na kumsakama Refa Eriksson.
Hata hivyo, Barca walishinda Mechi ya Marudiano huko Nou Camp Bao 3-1.
No comments:
Post a Comment