Kiongozi wa Extra Bongo, Ally Choky, akizungumzia uzinduzi huo ndani ya hoteli ya Atriums iliyopo Afrika Sana, Sinza.
Mratibu wa Burudani Dar Live, Luqman Maloto, akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Choky na Muumin Mwinjuma.
Extra Bongo wakiwa katika picha ya pamoja na Maloto katika hoteli ya Atriums.
Wanamuziki wa Extra Bongo (kutoka kulia) Sharapova, Super Nyamwela na Titi Mwinyi wakijiandaa kutoa burudani kidogo.
…Titi, Super Nyamwela na Sharapova wakionyesha mbwembwe zao kwa wanahabari (hawapo pichani).
Mnenguaji wa Extra Bongo, Sharapova akiwa katika pozi.
Titi Mwinyi katika picha ya pozi.
Banza Stone mmoja wa vivutio katika uzinduzi huo wa kesho.
Titi, Nyamwela na Sharapova wakiwa katika pozi.
Wanamuziki wa Extra Bongo wakipozi pamoja na Muumin Mwinjuma kwenye ukumbi wa hoteli ya Atriums iliyopo Afrika Sana, Sinza.
HAYAWI hayawi, sasa yamekuwa! Ule uzinduzi wa albamu ya ‘Mtendwa Akitendewa’ kutoka bendi ya Extra Bongo leo utafikia kilele ambapo watadondosha bonge la shoo katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem.
Akizungumzia
maandalizi ya mwisho kuelekea shoo ya albamu hiyo katika hoteli maarufu
ya Atriums iliyoko Afrika Sana, Sinza, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
wa Extra Bongo, Ally Choky, alisema kila kitu kinaenda sawa na hivi
sasa kilichobaki ni kudondosha mashambulizi siku ya kesho usiku.
Burudani
hiyo itanoga zaidi kutokana na kusindikizwa na wakali wa Bongo Fleva
kina Amin na Linah, Makhirikhiri wa Bongo, Bendi ya Mashujaa, TOT Band
chini ya ‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa.
Kiingilio kitakuwa ni sh. 6,000 tu.
No comments:
Post a Comment