MKURUGENZI Mkuu wa Kampuni ya usambazaji wa filamu za Kiswahili Lufingo Exaud amesema kuwa wameingiza mtaani filamu yao mpya ijulikanayo kwa jina la “Xdent” ambayo imeshilikisha wasanii mbalimbali wenye majina katika filamu hiyo utakutana na King Majuto, Muhogo Mchungu, Lufingo, Mzee Pembe na wasanii mbalimbali waliobobea katika sanaa hii ya filamu nchini.
filamu hiyo iliyorekodiwa kwa ubora wa hali ya juu na umakini mkubwa yenye mafundisho ndani yake itakuwa chachu kwa jamii kujirekerbisha katika maisha yao ya kila siku kwa sasa filamu hiyo inapatikana maduka yote yanayouza kanda za kiswahili nchini tanzania na mikoa yote kiujumla hivyo wapenzi wa filamu waende kununua DVD halali ili waendelee kukuza kipato cha wasanii nchini filamu hiyo ambayo imewashilikisha wasanii wengi wakubwa imekuwa ikigombaniwa sokoni kutokana na ubora wake pamoja na wasanii wenyewe jinsi walivyo onesha uwezo mkubwa wa kuitendea haki filamu hiyo.
No comments:
Post a Comment