Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemwahidi ushirikiano Rais wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi.
Ahadi
hiyo imetolewa leo (Februari 21 mwaka huu) makao makuu ya CAF jijini Cairo na
Rais wa shirikisho hilo Issa Hayatou alipokutana na Rais Malinzi aliyekwenda
kujitambulisha huko.
Utambulisho
wa Rais Malinzi kwa Rais Hayatou uliongozwa na mtangulizi wake Leodegar Tenga ambaye
aliiongoza TFF kwa vipindi viwili kuanzia 2004 hadi 2013.
Tenga
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na Mwenyekiti wa Baraza la
Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), alimweleza Rais
Hayatou kuwa uchaguzi wa TFF ulikuwa mzuri.
Aliongeza
kuwa alimkabidhi kijiti Rais Malinzi kwa maridhiano na ana imani na uongozi
wake.
Rais
Hayatou alimpokea Rais Malinzi na kuahidi kuendelea kuipa Tanzania ushirikiano
hasa katika maeneo ya utawala, ufundi na kuboresha miundombinu ya kuendeleza
mpira wa miguu.
Kwa
upande wake, Rais Malinzi alisema TFF itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa
CAF ili kuhakikisha kiwango cha mpira wa miguu nchini Tanzania kinakuwa.
Baadaye
mchana, Rais Malinzi alipata chakula cha mchana pamoja na wajumbe wote wa
Kamati ya Utendaji ya CAF.
No comments:
Post a Comment