Michuano
ya mikoa katika mpango maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
kuboresha Taifa Stars inaanza kutimua vumbi kesho kwa
mechi nne.
Mechi
rasmi ya ufunguzi wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager
itakuwa kati ya Ilala na Temeke. Mechi hiyo ya kundi G itachezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume kuanzia saa 9.30 alasiri.
Kundi
A kutakuwa na mechi kati ya Pwani na Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini mjini
Mlandizi wakati Kusini Unguja na Kaskazini Unguja zitacheza kwenye Uwanja wa
Mao Tse Tung mjini Unguja katika kundi H.
Kusini
Pemba na Kaskazini Pemba zitacheza mechi ya Kundi I katika Uwanja wa Gombani
kisiwani Pemba.
Mechi
za keshokutwa (Februari 23 mwaka huu) ni Simiyu itacheza na Shinyanga mjini
Bariadi katika kundi E. Nayo Ruvuma itacheza na Njombe kwenye Uwanja wa Majimaji
mjini Songea katika kundi D.
Kundi
C ni Tanga na Kilimanjaro kwenye Uwanja wa Mkwakwani wakati Kagera itacheza na
Geita kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika kundi B. Mtwara itacheza na
Lindi kwenye Uwanja wa Nangwanda mjini Mtwara katika kundi F.
Wang’amuzi
40 wa vipaji tayari wamesharipoti kwenye vituo vya mechi hizo kwa ajili ya
kufanya kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment