MENEJA
wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema Msimu wao mzuri ndani ya England
umewapa imani kubwa kuwa watawatoa Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich,
kwenye Mechi zao za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL, UEFA CHAMPIONS
LIGI.
Arsenal, kwenye Ligi Kuu England, wapo Nafasi ya Pili Pointi 1 nyuma ya Vinara Chelsea na pia wapo kwenye Robo Fainali ya FA CUP ambayo watacheza na Everton.
leo Jumatano Usiku watakuwa kwao Emirates kucheza na Bayern Munich kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL.
Lakini, Msimu uliopita, kwenye hatua kama hii na Mechi kama hii, walinyukwa Bao 3-1 na Bayern Munich Uwanjani Emirates na licha ya kushinda 2-0 kwenye Marudiano huko Munich, Arsenal walitupwa nje kwa Bao za Ugenini.
Msimu huu, Wenger anataka wakwepe hatima iliyuowakuta Msimu uliopita na amesisitiza: “Tuna Timu yenye ari kubwa, nia kubwa ya kufanya vyema na iko pamoja kwa kila kitu. Imani hujengwa na matokeo na kwa hilo tuna nguvu zaidi. Mwaka Jana tulitolewa kwa Bao za Ugenini, hivyo ni muhimu tusiruhusu Bao. Matokeo mazuri Nyumbani ndio muhimu kwa Mechi hizi.”
Wenger alifafanua: “Safari hii tupo vyema kiisaikolojia kupita Mwaka Jana. Tulifungwa na Blackburn tukiwa Nyumbani kwenye FA CUP na hilo lilituvunja moyo lakini Mwaka huu tumeshinda dhidi ya Liverpool na tuna nia kubwa ya kuifunga Bayern Munich.”
Kwenye Mechi ya Jumatano na Bayern, Wenger amedokeza Tomas Rosicky atambadili Mikel Arteta ambae yuko Kifungoni.Wachezaji wa Timu ya Arsenal wakifanya mazoezi hii leo kujiweka sawa na mtanange wao na Bayern Munich jumatano.Bosi Arsene Wenger leo hii kwenye mazoezi Ni patashika kati ya Arsenal FC v Bayern Munich jumatano
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA/MATOKEO
Jumanne Februari 18
Manchester City 0 v FC Barcelona 2
Bayer 04 Leverkusen 0 v Paris Saint-Germain 4
Jumatano Februari 19
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich

No comments:
Post a Comment