RAIS wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amezindua programu ya kutoa
elimu ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana iitwayo
Ishi Huru. Programu hiyo iliyozimduliwa jana (Januari 10 mwaka huu)
jijini Dar es Salaam iko chini ya taasisi ya Africa Inside Out
inayoongozwa na Rebecca Young wakati washirika (partners) ni TFF na
kampuni ya Rhino Resources ya Marekani. Rais Malinzi amesema matumizi ya
dawa za kulevya nchini yamekuwa yakiongezeka, hivyo kuwa kikwazo kwa
maendeleo ya vijana ambapo ameipongeza Africa Inside Out kwa programu
hiyo kwa vile itazuia vijana wengi kujiingiza katika matumizi ya dawa
hizo. “Moja athari kubwa za matumizi ya dawa za kulevya ni kupata
maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na kuchangia sindano za
kujidunga dawa hizo. “TFF tutatoa ushirikiano wa kutosha katika programu
hii. Lakini pia tutaingiza Ishi Huru katika programu zetu za mpira wa
miguu kwa vijana. Tutahamasisha jamii katika kupambana na dawa za
kulevya,” amesema. Katika uzinduzi huo, pia Rais Malinzi alizundua
semina ya waelimishaji na kuwaeleza kuwa wamepata fursa hiyo kwa vile ni
vijana wanaojituma, hivyo watafikisha vizuri ujumbe wa Ishi Huru katika
shule na vituo vya vijana nchini.
No comments:
Post a Comment