Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, January 12, 2014

LIVERPOOL ILIPOISAMBARATISHA STOKE CITY 5-3 NA KUENDELEA KUKALIA NAFASI YA NNE


Suarez akishangilia bao lake la pili katika dakika ya 71 na kufanya bao kuwa 4-2 katika kipindi cha pili. Timu ya Stoke City leo ikiwakaribisha Majogoo Liverpool kwao wametoka nyuma ya bao 2-0 na kufufuka kwa kusawazisha bao zote mbili katika kipindi cha kwanza cha dakika 45. Bao za Liverpool zimefungwa na
Ryan Shawcross katika dakika ya tano bao la kujifunga huku bao la pili likifungwa na  Luis Suárez katika dakika ya 32 kipindi cha kwanza. Stoke waliongeza bidi zaidi na hatimae kusawazisha bao hizo katika dakika ya 39 na mchezaji wake matata Peter Crouch  huku bao la pili likisawazishwa katika dakika za lala salama za kipindi cha kwanza katika dakika ya 45 na Charlie Adam.

Kipindi cha pili dakika ya 51 Steven Gerrard akaipatia bao la kuongoza la tatu timu ya Liverpool kwa mkwaju wa penati. Dakika ya 71 Luis Suarez akaipachikia bao Liverpool likiwa la pili kwake na kufanya bao kuwa 4-2 dhidi ya wenyeji Stoke City wanaoshika nafasi ya 12 wakiwa na pointi 22 tu katika michezo 21. Bao la tano limefungwa na Daniel Sturridge
dakika ya 87 baada ya kufanya Juhudi zake binafsi na kuiwasha bao Stoke City katika dakika za lala salama.Charlie Adam akiifungia bao la kusawazisha timu yake ya Stoke katika dakika ya 45  kipindi cha kwanzaCharlie Adam akipongezwa baada ya kusawazisha bao mwishoni mwa kipindi cha kwanza. Jon Walters wa Stoke City kwenye patashika na Aly Cissokho wa Liverpool

No comments:

Post a Comment