Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 24, 2014

KUNDI LA MAKHIRI KHIRI, AMINI KUMSINDIKIZA BANZA STONE JUMAMOSI


Na Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' Amin na kundi la Sanaa la Makhirikhiri wa bongo ni miongoni mwa burudani
zitakazosindikiza onyesho maalumu la 'Usiku wa Banza Stone' la bendi ya Extra Bongo 'Next Level' Wazee wa Kizigo kwa ajili ya kumtambulisha mtunzi na mwimbaji wake Ramadhani Masanja 'Le General Banza Stone' anayerejea upya jukwanii Jumamosi hii ndani ya Meeda Club Sinza jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa msemaji wa bendi hiyo Juma Kasesa, maandalizi ya onyesho hilo yamekamilika na tayari Banza ameanza mazoezi makali ya kufua sauti yake tayari kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi waliokuwa wame-mis sauti na tungo zake.

Kwa muda wa miezi mitatu Banza alikuwa yu mgonjwa hali iliyomsababishwa kushindwa kupanda jukwaani kabla ya mwishoni
mwa mwaka jana kujikongoja na kushiriki kwenye ziara ya 'Mafahari Watatu' katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwa na bendi hiyo lakini akalazimika kupewa mapumziko ili aweze kufanya mazoezi na kula kwa mpangilio ili aweze kuimarisha afya yake.
Alisema, Amin na Makhirikhiri wa Bongo ni sehemu tu ya burudani zitakazopamba 'usiku wa Banza Stone' kwani kutakuwa na vikundi vingine vya sanaa vitakavyonogesha onyesho ambapo mara baada ya onyesho hilo wataendelea kumtambulisha Banza katika kumbi mbalimbali za burudani jijini Dar es Salaam kabla ya kufanya ziara nyingine katika baadhi ya Mikoa.

No comments:

Post a Comment