KLABU
ya Cardiff City imethibitisha kumteua Ole Gunner Solskjaer kuwa meneja
mpya wa klabu hiyo. Solskjaer anachukua nafasi ya mikoba ya Malky Mackay
ambaye alitimuliwa na mmiliki wa klabu hiyo ya Wales Vincent Tan.
Toka
kutimuliwa kwa Mackay, David Kerslake ndiye aliyepewa mikoba ya muda ya
kuinoa klabu hiyo na kuingoza kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya
Sunderland na baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal.
Akihojiwa
mara baada ya uteuzi huo Solskjaer ambaye alikuwa mshambuliaji wa
zamani wa Manchester United amesema hiyo ni changamoto mpya kwake na
anategemea kuisaidia Cardiff kupiga hatua nyingine.
Malky Mackay (kulia) aliyetimliwa hivi karibuni.
Ole Gunnar Solskjaer akipozi kupata picha na jezi ya Cardiff City baada
ya kutambulishwa rasmi huku wadau wengi wakishangaa uteuzi huo!

Solskjaer akiteta na waandishi wa habari na vyombo vya habari leo baada ya uteuzi wake kwa kuinoa Cardiff
Solskjaer yeye amefurahia uteuzi huo

Enzi hizo: Solskjaer (kulia) akiwa na kocha wa zamani wa United Sir Alex Ferguson.
Solskjaer akiwa chini ya Ferguson enzi hizo huko Manchester United
No comments:
Post a Comment