Champions League
- Venue: Old Trafford
- Date: 10 December
- Kick-off: 1945 GMT
Walinzi Nemanja Vidic, Patrice Evra na Chris Smalling wako mashakani
kuanza kwa upande wa Manchester United dhidi ya Shakhtar Donetsk,
Marouane Fellaini alikosekana mazoezini hapo jana Jumatatu.
Kiungo huyo amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo na huenda
Shinji Kagawa akawepo baada ya kukosekana katika mchezo wa ligi dhidi ya
Newcastle kwa taarifa ya kuwa alikuwa anaumwa.
United tayari imefuzu kwa hatua ya mtoano lakini inahitaji alama hii kuongoza kundi.
- United imeshinda mara tano katika jumla ya michezo 12 ya ligi iliyopita nyumbani Old Trafford, ikifunga magoli manane.
- Shakhtar wana alama tano wakiongoza ligi ya kwao wakielelea katika mapunziko ya majira ya baridi na mchezo wa ligi wa kwanza utakuwa mwezi March.
USHINDI kwa Shakhtar ndani ya Old Trafford, utakuwa ni kwanza ndani
ya England, na utawezesha kikosi cha Mircea Lucescu kuipiku United
katika kilele cha kundi A.
No comments:
Post a Comment