Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, December 10, 2013

KOCHA WA BARCELONA GERARDO MARTINO AMCHANA NEYMAR

Kocha wa Barcelona Gerardo Martino amempa changamoto Neymar da Silva Santos Júnior kuboresha kiwango na uwezo wake wa kufunga wakati huu ambapo klabu hiyo inaendelea kukosa huduma ya mshambuliaji Lionel Messi.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil mpaka sasa amemudu kufunga mabao 5 tu katika jumla ya michezo ya kimashindano 20 ndano ya Blaugrana tangu ajiunge nayo kwa euro milioni €57 akitokea klabu ya Santos wakati wa uhamisho wa majira ya kiangazi licha ya kupiga pasi za mwisho tisa zilizo zaa magoli.

Wakati Messi akiendelea kuwa nje ya uwanja kutokana na matatizo ya msuli Martino amemtaka Neymar kuboresha ufungaji wake licha ya msaada wake mkubwa tu uwanjani ingawaje pia ameweka wazi kuwa Mbrazil huyo hafanini na Messi katika ufungaji wao.

"But at the moment the only question about Neymar is his finishing.

Barcelona usiku huu itakuwa ikikutana dhidi ya Celtic wakihitaji matokeo mazuri ambayo yatawafanya kuweza kuongoza kundi ambapo bosi Martino ametaka kikosi chake kupigana ili kuweza kushinda kufuatia matokeo mabaya ya hivi karibu.

No comments:

Post a Comment