Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 13, 2013

KILIMANJARO STARS ILIPOAMBULIA NAFASI YA NNE CHALENJI

Na Mahmoud Zubeiry, Nairobi
NG’OMBE wa masikini hazai, huo ni msemo maarufu wa wahenga ambao leo umedhihirika Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya- baada ya timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ kukosa hata nafasi ya tatu katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kufungwa na Zambia kwa penalti 6-5 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.
Wachezaji wa Zambia wakishangilia baada ya kuiua Stars

Kipa Ivo Mapunda alipangua penalti mbili za Wazambia, Justin Zulu na Kondwani Mtonga, lakini Haroun Chanongo, Mrisho Ngassa na Nahodha Kevin Yondan wote wakakosa penalti zao zikiokolewa na kipa wa Chipolopolo, Joshua Titima.
Waliofunga penalti za Zambia ni Felix Katongo, Ronald Kampamba, Bronson Chama, Julius Situmbeko, Rodrick Kabwe na Kabaso Chongo, wakati za Stars zilifungwa na Mbwana Samatta, Erasto Nyoni, Himid Mao, Amri Kiemba na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Katika mchezo huo, Zambia walitangulia kupata bao dakika ya 52 kupitia kwa Ronald Kampamba kabla ya Mbwana Samatta kufunga bao zuri mno dakika ya 65 akiisawazishia Stars.
Mchezo huo ulisimama kwa dakika sita, dakika ya 88 kufuatia Polisi kufyatua mabomu ya machozi wakipambana na mashabiki wa Kenya waliokuwa wanataka kuingia bure uwanjani.
Wachezaji walianza kuanguka mmoja mmoja kutokana na kuzidiwa na hewa ya mabomu, hivyo marefa wakasimamisha mchezo kabla ya kuanza tena dakika sita baadaye. 
Kwa matokeo hayo, Stars inaondoka Challenge ya 2013 na nafasi ya nne kama mwaka jana mjini Kampala, Uganda ilipofungwa kwa penalti pia na Zanzibar katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
 
Mshambuliaji wa Tanzania Bara, 'Kilimanjaro Stars', Mbwana Samatta akienda chini bada ya kukwatuliwa na wachezaji wa Zambia katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge jioni ya leo Uwanja wa  Nyayo, Nairobi, Kenya. Zambia ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90. 
Mbwana Samatta akiwania mpira wa juu dhidi ya Rodrick Kabwe wa Zambia kushoto

Mbwana Samatta akichuana na Nahodha wa Zambia, Bronson Chama kulia
Mrisho Ngassa akimpiga tobo beki wa Zambia, Rodrick Kabwe
Mrisho Ngassa akitafuta mbinu za kumtoka Sydney Kalume wa Zambia kulia
Felix Katongo wa Zambia akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Stars, Athumani Iddi 'Chuji'
Haikuwa riziki; Kipa Ivo Mapunda na beki wake Said Mourad wakitoka uwanjani baada ya mechi
Walikosekana; Kiungo Frank Domayo kushoto akiwa na mshambuliaji Thomas Ulimwengu wakifuatilia mechi hiyo jukwani
Wachezaji wa zamani Tanzania, Kitwana Manara 'Popat' kushoto na Joe Kadenge wa Kenya kulia walikuwepo Nyayo
Wachezaji wa zamani wa Tanzania
Erasto Nyoni akimtoka Felix Katongo
Salum Abubakar 'Sure Boy' akimtoka Rodrick Kabwe
Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa Zmbia
Haroun Chanongo kulia akimtoka Kabaso Chongo
Wachezaji wa Stars wakinawa maji baada ya mchezo kusimama kutokana na kulipuliwa kwa mabomu ya machozi na Polisi dakika ya 88 wakipambana na mashabiki wa Kenya waliotaka kuingia uwanjani bure
Kujiokoa dhidi ya mabomu
Mrisho Ngassa kulia na Amri Kiemba kushoto wakikimbia mabomu. Mchezo ulisimama dakika ya 88 hadi baada ya dakika sita ukaendelea

No comments:

Post a Comment