KIKOSI cha
Azam FC, kinatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Januari mosi, kuelekea visiwani
Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Akizungumza
jijini, Meneja wa Azam FC, Jemadari Said Kazumari,alisema Azam itaondoka na wachezaji 33 wakiwemo
waliopandishwa kutoka timu B na huenda Humphrey Mieno akakosekana kwa vile bado
hajawasili kujiunga na mazoezi
“Timu
inatarajiwa kuondoka Januari mosi kwenda Zanzibar kuanza kutetea ubingwa wake
wa Mapinduzi lakini tunaweza kumkosa Mieno kwani bado hajafika kambini na
tumekuwa tukimtumia ujumbe wa barua pepe na sms kumuuliza kulikoni amechelewa,
lakini hajibu, hivyo hatuelewi sababu iliyomchelewesha,”alisema.
Jemadari
alisema Mieno alipewa ruhusa ya awali lakini ilipomalizika aliwasiliana na uongozi
na kusema ana matatizo ya kifamilia, hivyo akaongezewa muda ambao pia umeisha.
Pia Jemadari
alisema wana mchezaji mpya mazoezini kutoka Don Bosco ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Djunes Kayanda aliyewahi pia kuchezea Zanaco ya
Zambia.
Jemadari
amesema mshambuliaji huyo ni kijana mdogo ana umri wa miaka 19 ingawa kwa sasa
hawezi kusajiliwa, lakini uongozi umempa muda zaidi kuendelea kuangalia kiwango
chake.
Azam ina
wachezaji watano wa kigeni, ambao ni kiungo Kipre Balou na washambuliaji Kipre
Tchetche na Muamad Ismael Kone wote kutoka Ivory Coast pamoja na Mganda Brian
Umony na Mkenya Humphrey Mieno.
Kone
amesajiliwa msimu huu kuchukua nafasi ya beki Mkenya, Joackins Atudo
aliyemaliza mkataba wake.
Kikosi
kinachotarajiwa kuondoka ni wachezaji; Aishi Manula,
Abdallah Karihe, Aggrey
Morris, Bryson Nkulula,
Brian Umomy,
David Mwantika,
Erasto Nyoni,
Farid Mussa, Gaudence Mwaikimba,
Gadiel Michael, Himid Mao,
Ibrahim Mwaipopo na Ismail Gambo
Wengine ni
Jabir Aziz, John Bocco, Joseph Kimwaga, Kelvin Idd, Kipre Tchetche,
Kone Ismael Mouhamed,
Hamis Mcha, Luckson Jonathan,
Bolou Kipre, Malika Ndeule, Mudathir Yahya, Mwadini ali mwadini, Reyna Mgungila, Said Moradi
samih Nuhu,
Swalehe Abdallah, Wandwi
Jackson,
Waziri Salum,
Salum Abubakar,
Humphrey Mieno na Hamadi Juma
Wakati
viongozi watakaoongozana na timu ni kocha Mkuu Joseph Omog
na kocha msaidizi Kalimangonga
Ongala, Mwnandi Mwankemwa ambaye ni daktari wa timu, Jemadari Said ambaye ni
meneja wa timu.
Viongozi
wengine ni Ibrahim Shikanda, Idd Abubakar, Vivek Nagul,
Vicent Juma, Twalibu Mbaraka,
Yusuf Nzawila
na Swalehe Awadh.
No comments:
Post a Comment