WANACHAMA wa Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA) wametakiwa
kulipa ada za unachama mapema ili kusaidia chama kutekeleza malengo yake kwa
wakati.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa TAFCA, Michael Bundala
wakati akifanya mahojiano na gazeti hili katika ofisi za chama hicho zilizopo
Karume, Dar es Salaam.
Bundala alisema kuwa kwa sasa TAFCA ina wanachama 300
Tanzania nzima na kuwataka makocha wote waliosomea kujiandikisha kwenye ofosi
za wilaya na mikoa na kulipa ada ili wawe wanachama hai wapate fursa
zinazotolewa na cham,a chao.
“TAFCA tuna wanachama 300 nchini idadi ambayo ni ndogo
kulinganisha na idadi ya makocha waliopo nchini ambao tayari wamesomea hivyo tunawataka kulipa ada ya uanachama
ambayo ni 24,000 kwa mwaka”, alisema Bundala.
Bundala alisema asilimia 40 ya ada hiyo inabaki kwenye ofisi
za mkoa kusaidia shughuli za ofisi na asilimia 60 inaletwa TAFCA makao makuu.
Pia alisema wana mpango wa kuendeleza mafunzo ya ukocha
katika mikoa mipya ili kupata makocha ambao wataendeleza soka katika mikoa
hiyo.
No comments:
Post a Comment