Wachezaji wa Yanga wakishangilia mabao yao waliyofunga leo |
Kikosi cha mtibwa |
Kikosi cha Yanga |
Daktari wa Yanga Nassoro Matuzya akimganga Simon Msuva |
Kocha wa Yanga Ernie Brandts akizungumzia mchezo wao na Mtibwa mara baada ya mchezo kumalizika |
Kocha wa Mtibwa, Mecky Mexime akizungumzia mchezo wao dhidi ya Yanga mara baada ya mchezo kumalizika |
Paul Ngalema wa Yanga akiondoa mpira eneo la hatari huku Hamis Kiiza akimkimbilia |
YANGA SC imebakisha pointi
tatu kuwafikia watani wao wa jadi, Simba SC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia
ushindi wa mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Yanga sasa imetimiza pointi 12 na kupanda hadi nafasi ya pili, wakati Simba SC inaendelea kukaa kileleni kwa pointi 15, baada ya timu zote kucheza mechi saba.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Isihaka Shirikisho, aliyesaidiwa na Mohamed Mkono na Kudra Omary wote wa Tanga, hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao hayo 2-0.
|
Yanga ilijipatia bao kupitia
kwa mshambuliaji Mrisho Ngassa aliyepokea pasi ndefu ya Athumani Iddi ‘Chuji’
na kumzidi maarifa beki Salvatory Ntebe kabla ya kupiga shuti lililomshinda kipa
Hussein Sharrif ‘Casillas’ dakika ya sita.
Mrisho Ngassa pia alimtoka vyema beki wa pembeni wa Mtibwa, Paul Ngalema na kupiga krosi maridadi iliyounganishwa nyavuni na Didier Kavumbangu dakika ya 24.
Mrisho Ngassa pia alimtoka vyema beki wa pembeni wa Mtibwa, Paul Ngalema na kupiga krosi maridadi iliyounganishwa nyavuni na Didier Kavumbangu dakika ya 24.
Kipindi cha pili, Mtibwa walirudi wakiwa imara zaidi na kuonyesha upinzani kwa Yanga, wakijitahidi kuwadhibiti vizuri washambuliaji wa timu hiyo na pia kushambulia.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite/Juma Abdul dk77, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva/Nizar Khalfan dk59, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Said Bahanuzi dk80.
Mtibwa Sugar; Hussein Sharif, Hassan Ramadhan, Paul Ngalema, Salvatory Ntebe/Dickson Daud dk33, Salim Abdallah, Shaaban Nditi, Ally Shomary, Awadh Juma, Mussa Mgosi/Juma Luizio dk66, Shaaban Kisiga na Vincent Barnabas/Masoud Mohamed dk37.
Katika mchezo mwingine, Mgambo JKT imefungwa nyumbani 1-0 na Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga bao pekee la Peter Michael dakika ya 62.
No comments:
Post a Comment