Waziri
wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akimkabidhi bendera ya
taifa leo Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara
zoezi hilo lilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo tayari
kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe
yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba, Kati kati ni
muandaaji wa shindano hilo nchini Bi. Maria Sarungi.
Na. Mwandishi wetu
Mrembo
wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara amekabidhiwa
bendera leo na waziri wa mali asili na utalii mheshimiwa Balozi Khamis
Kagasheki.
Zoezi
hili limefanyika katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa
safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe yatakayofanyika
Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba.
Akimkabidhi bendera huku akimpongeza waziri Kagasheki pia amemtakia mafanikio mema huko aendako.
Betty
pia aliwaahidi watanzania kuwa mbali na kurudi na ushindi lakini pia
ataenda kuitangazia dunia kuacha kutumia nakshi(Mapambo) yanayotumia
pembe za ndovu ili kumaliza tatizo la ujangili nchini.
Zoezi la kukabidhiwa bendera lilifanyika likishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.
Mashindano
ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na hifadhi ya Taifa Tanapa
na Mrembo Betty Boniface ameshaanza kutangaza hifadhi hizi kwa njia
mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment