Na Mwandishi Wetu.Morogoro
NAIBU waziri wa habari utamaduni na Michezo Amos
Makalla ameikabidhi timu ya taifa ya pool table bendera ya taifa kwaajili ya
kwenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano
ya afrika mashariki nchini Malawi,ambapo aliwataka kwenda kuitangaza
nchi kwa mema.
Makala
alikabidhi bendera hiyo jana mjini
Morogoro na kuwahimiza wachezaji hao kuhakikisha wanakuwa raia wema ili wengine
waweze kuiga kutoka kwao sambamba na kuonyesha umoja na ushirikiano.
Alisema Serikali imeanza kuutambua mchezo huo na
kuupa ushirikiano hivyo kuipongeza kampuni ya TBL kupitia bia yake ya safari
lager ambao ndiyo wadhamini wakubwa wa mchezo huo.
“ Hongereni TBL kwa kazi nzuri mnayoifanya huu mchezo
ulikuwa haufahamiki kabisa na sasa unajulikana na kupendwa ni kazi kubwa ambayo
mmeifanya inayostahili kuigwa na makampuni mengine” Alisema Naibu Waziri huyo.
Naye Mwalimu anaeinoa timu hiyo alisema anaishukuru timu hiyo kwa
kuwa imekuwa ikionesha nidhamu ya hali ya juu tangu wakiwa kambini, nakwamba
timu imejiandaa vya kutosha na wanauhakika wakurudi na ushindi
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chama cha mchezo
wa pool table Tanzania (TAPA) Fredy
Mushi aliiomba serikali iuangalie mchezo huo badala ya kungalia michezo
mingine, nakwamba kufanya hivyo kutawawezesha wachezaji kuwa na ari ya kufanya
vyema zaidi wakati wamashindano kama haya.
Aidha wachezaji wanaokwenda kushiriki michuano hiyo
nchini Malawi ni , Kampten watimu hiyo Vernace Charles, Omary Akida, Festo
yohana, Mohamed Idd, Mercxedek Amedius,Godfrey Swai, Abdala Husein, na Patrick
Mnyanguzi.
Mashindano hayo ambayo yanataji kuanza kutimua vumbi
Oktoba 23 hadi 26 yanatarajia kushirikisha nchi 14 kutoka afrika ambazo ni Kenya , Tanzania,Afrika ya
Kusini,Zambia, Lesotho,Kongo, Swazland, Ghana,,Nigeria, Misri, Morocco,
Namibia, Msumbiji, na Mwenyeji Malawi.
No comments:
Post a Comment