Bosi
wa Bayern Munich Pep Guardiola amesema wachezaji wake wanapaswa
kukubali maamuzi yake endapo mambingwa hao wa Ulaya na Ujerumani
watakuwa wanataka kutetea taji lao la Bundasliga msimu huu.
Bayern, ambao walishinda taji ya German Cup na ligi ya mabingwa
Ulaya msimu uliopita wanajipanga kuelekea kucheza mchezo wao wa 34
nchini Ujerumani bila kufungwa hapo kesho Jumamosi.
Watakuwa ni wenyeji wa Mainz katika dimba la Allianz Arena.
Ratiba ya michezo ya Kesho Jumamosi
- Bayern Munich v Mainz (14:30 BST)
- Borussia Dortmund v Hannover (14:30 BST)
- Real Madrid v Malaga (15:00)
- Paris St-Germain v Bastia (16:00)
- Osasuna v Barcelona (19:00)
- Sochaux v Monaco (13:00)
- Fiorentina v Juventus (14:00 BST)
- Torino v Inter Milan (19:45)
Amenukuliwa Guardiola akisema
"Tutapigania
taji la Ujerumani mpaka mwisho wa msimu mchezo lakini endapo kila
mchezaji atakubaliana na maamuzi yangu, vinginevyo tutapata matatizo"
Vinara hao wa Bundasliga bado hawajafungwa wakiwa na alama moja
tofauti na wanaowafuata Borussia Dortmund wakiwa wanamichezo sita ya
ushindi katika michezo yao.
Endapo wataepuka kichapo kutoka kwa Mainz, Bavarians watakuwa na
michezo miwili nje ya uwanja wa nyumbani kuelekea kuifikia rekodi ya
Hamburg ya kutokupoteza michezo 36 rekodi waliyo iweka mwezi Januari
1983.
No comments:
Post a Comment