Magari
yenye shughuli maalumu tu ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanja wakati
wa mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa keshokutwa (Jumapili) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi
itaanza saa 10 kamili jioni, na kila timu inaruhusiwa kuingia na magari
matatu tu; gari la timu na mengine mawili ya viongozi. Ukaguzi wa
kuingia uwanjani ni kwa watu wote, kwani utaratibu huo si wa
kumdhalilisha mtu bali lengo lake ni kuhakikisha usalama.
Vilevile
watu hawataruhusiwa kuingia uwanjani na mifuko ya aina yoyote ikiwemo
mabegi, isipokuwa kwa waandishi wa habari wanaotumia mabegi hayo kwa
ajili ya kubebea kamera zao. Pia hakuna wafanyabishara watakaoruhusiwa
kufanya biashara katika maeneo yanayozunguka uwanja.
Kwa
washabiki watakaokuwa katika mazingira ya kuwa kero kwa wenzao wakiwemo
walevi hawataruhusiwa kuingia uwanjani, pamoja na wale wenye silaha
kama bastola ambapo wakikamatwa wafikishwa polisi na baadaye kufunguliwa
mashtaka kortini.
Barabara
ya Uwanja wa Taifa itafungwa kuanzia saa 2 asubuhi upande wa
Chang’ombe, hivyo washabiki wanatakiwa kununua tiketi zao mapema kesho
(Jumamosi) ambapo zitaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali kuanzia saa 4
asubuhi.
Vituo
hivyo ni mgahawa wa City Sports Lounge, Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora,
Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa
Uhuru, mgahawa wa Brake Point uliopo Kijitonyama na BMM Salon iliyoko
Sinza Madukani.
No comments:
Post a Comment