Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetangaza
orodha ya mwisho ya wagombea wa uchaguzi wa TFF na wa Bodi ya Ligi (TPL
Board) utakaofanyika baadaye mwezi huu.
Uchaguzi
wa Bodi ya TPL utafanyika Oktoba 25 mwaka huu wakati ule wa TFF
utafanyika Oktoba 27 mwaka huu. Kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa TPL
Board na ule wa TFF zimeanza leo (Oktoba 18 mwaka huu) zitamalizika siku moja kabla ya uchaguzi saa 10 kamili alasiri.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni amewataja wagombea kwa upande
wa TPL Board kugombea uenyekiti ni Hamad Yahya Juma (Mtibwa Sugar),
Makamu Mwenyekiti ni Said Muhammad Said Abeid (Azam). Wanaowania ujumbe
wa Bodi ya Uendeshaji ni Kazimoto Miraji Muzo (Pamba) na Omary Khatibu
Mwindadi (Mwadui).
Wagombea
kwenye uchaguzi wa TFF ni Athuman Jumanne Nyamlani na Jamal Emily
Malinzi (Rais), Imani Omari Madega, Ramadhan Omar Nassib na Wallace
Karia (Makamu wa Rais).
Kwa
upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Kalilo Samson (Kanda namba
1- Geita na Kagera), Jumbe Odessa Magati, Mugisha Galibona, Samwel
Nyalla na Vedastus Lufano (Kanda namba 2- Mara na Mwanza), Epaphra Swai
na Mbasha Matutu (Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu).
Ali
Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omar Walii Ali (Kanda namba 4- Arusha na
Manyara), Ahmed Idd Mgoyi na Yusuf Hamis Kitumbo (Kanda namba 5- Kigoma
na Tabora), Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo (Kanda namba 6-
Katavi na Rukwa), Ayoub Shaibu Nyenzi, David Samson Lugenge, John
Exavery Kiteve, Lusekelo Elias Mwanjala (Kanda namba 7- Iringa na
Mbeya).
James
Patrick Mhagama na Stanley William Lugenge (Kanda namba 8- Njombe na
Ruvuma), Athuman Kingombe Kambi, Francis Kumba Ndulane na Zafarani Mzee
Damoder (Kanda namba 9- Lindi na Mtwara), Hussein Zuberi Mwamba, Stewart
Ernest Masima, Charles Komba (Kanda namba 10- Dodoma na Singida), Farid
Nahdi, Geofrey Irick Nyange, Juma Abbas Pinto, Riziki Juma Majala) na
Twahil Twaha Njoki (Kanda namba 11- Morogoro na Pwani).
Davis
Elisa Mosha, Khalid Abdallah Mohamed (Kanda namba 12- Kilimanjaro na
Pwani), Alex Crispine Kamuzelya, Kidao Wilfred Mzigama, Muhsin Said
Balhabou na Omary Isack Abdulkadir (Kanda namba 13- Dar es Salaam).
Mbwezeleni
amewataka wagombea kufanya kampeni bila kukashfu wenzao, kwani Kanuni
ya Uchaguzi za TFF toleo la 2013 inatoa fursa kwa Kamati ya Uchaguzi
kuwaondoa wagombea wa aina hiyo kwenye uchaguzi.
No comments:
Post a Comment