Mwamuzi Israel Nkongo (wa tatu toka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja katika moja ya mechi alizowahi kuchezesha |
Watanzania
watatu ni miongoni mwa washiriki 30 walioteuliwa kuhudhuria kozi ya
wakufunzi ya waamuzi ya FUTURO III itakayofanyika Addis Ababa, Ethiopia
kuanzia Oktoba 5 hadi 10 mwaka huu.
Leslie
Leonard Liunda, Abdi Soud Mohamed na Israel Nkongo Mujuni ndiyo
watakaoshiriki katika kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Kozi
hiyo pia itakuwa na washiriki kutoka nchi nyingine tisa za Afrika. Nchi
hizo ni Gambia, Ghana, Kenya, Liberia, Nigeria, Seychelles, Sierra
Leone, Somalia na Uganda.
No comments:
Post a Comment