TIMU ya Friends Rangers ya Magomeni
jana iliwalaza mapema mashabiki wa Villa Scuad pia ya Magomeni baada ya
kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi daraja la kwanza uliochezwa Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikuwa na
ushindani kwa mashabiki a wachezaji pia kiasi cha kuonyeshana ubabe waziwazi
ulishuhudia Friends Rangers wakipata bao dakika ya nne kupitia kwa mshambuliaji
Credo Mwaipopo lakini Villa Scuad walifanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 11
kupitia kwa mshambuliaji Daniel Jemadari baada ya kupokea pasi toka kwa Gondwe
Andrew.
Baada ya Villa Scud kusawazisha bao
hilo Friends
Rangers walicharuka na kufanikiwa kuongeza bao la pili kupitia kwa
mshambuliajia Khalid Rubagula katika dakika ya 14 baada ya kutokea piga ni
kupige kwenye lango la Villa Scuad.
Kipindi cha pili kila timu
zilifanya mabadiliko hali iliyozidisha uimara wa kila timu huku ladha ya mchezo
ikiondoka kutokana na wachezaji wa Friends Rangers kupoteza muda kwa
kujiangusha mara kwa mara na kucheza rafu hali iliyosababisha beki Isihaka
Chambuli kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 78 baada ya kumkwatua
mshambuliaji wa Villa Scuad Najim Benjamin.
Pia kocha wa Friends Rangers Kheri Mzozo aliondolewa kwenye
benchi la ufundi baada ya kuonekana kupinga wazi maamuzi ya mwamuzi Omar Yusuph
baada ya kusimama na kwenda hadi kwa mwamuzi wa akiba pamoja na meza kuu na
kuanza kulalamika kwa sauti lakini cha kushangazaaskari polisi waliokuwepo
uwanjani hapo walishindwa kumwondoa hali iliyoacha maswali mengi kwa mashabiki.
Akizungumza baada ya mchezo kocha wa Villa Scuad, Bakari Idd
alimtupia lawama mwamuzi wa mchezo huo kwa kukubali vitendo vya ucheleweshaji
muda vilivyokuwa vikionyeshwa na viongozi wa Friends Rangers na wachezaji wao hata
pale alipoonyesha muda wa ziada kuwa dakika 4 lakini alitumia dakika mbili tu.
“Mwamuzi kachangia kuharibu mchezo kwani wachezaji wa Friends
Rangers walikuwa wanajiangusha na pale huduma inapoitwa daktari wao alikuwa anawakataza kubebwa na
huduma ya kwanza na mwamuzi hakuchukua hatua yoyote”, alisma Idd.
No comments:
Post a Comment