London, England
LICHA
ya Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kukubali kwamba mchakato wa usajili ni
tatizo kwake, ameonesha kiburi na ubinafsi mkubwa, baada ya kusisitiza kwamba
kamwe hatakubali kufanya kazi chini ya mkurugenzi wa soka.
Tottenham
ambayo jana iliwavaa wapinzani wao hao wa London, 'The Gunners’, yenyewe
ilimteua Franco Baldini kama mkurugenzi wa soka majira haya ya joto na kisha
kumpa Muitalia huyo jukumu zima la mchakato wa usajili.
Matokeo
yake ni Spurs kufanikiwa kuvunja rekodi yake ya usajili, kwa kusaini nyota bora
ikijiandaa kumkosa Gareth Bale.
Lakini
Arsenal imeshindwa kufanikiwa kuipata saini ya Luis Suarez na Wayne Rooney,
huku ikifanikiwa tu kuwasajili kwa uhamisho huru Yaya Sanogo na Mathieu Flamini
kuelekea dirisha la usajili linalofungwa leo saa sita usiku.
“Siwezi
kufanya kazi chini ya mkurugenzi wa soka kwa sababu wananunua wachezaji na
wanaposhindwa kucheza vema, unalaumiwa kwa kutowatumia ipasavyo,” alisema
Wenger.
“Sipingi
kutokuwa na mtu wa kunisaidia kununua, kuuza na kufanya mazungumzo, kwa sababu
sitaweza kufanya kila kitu. Lakini nadhani uamuzi wa mwisho mara zote lazima
ubaki kwa kocha kuamua nani asajiliwe na yupi auzwe kwa kuwa yeye ndiye
muwajibikaji kwa staili ya uchezaji na matokeo.”
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, huko England, Wenger aliongeza: “Ni kama kuandika
makala yako na mtu fulani aseme nitabadilisha hiki na hiki. Hutaweza
kukubaliana na hilo, simamia kile ulichokiandika! Ninasimamia matokeo ya timu
niliyoichagua. Kocha lazima awajibike kwa wachezaji wanaosajiliwa.”
Lakini
Wenger alipoulizwa kuwa anabeba mzigo mkubwa sana kwa kujaribu kuiandaa timu na
kuhusika moja kwa moja katika usajili, Mfaransa huyo, 63, alikubali kuwa
inaweza kuwa ngumu.
“Siwezi
kukataa kuwa mchakato wa usajili ni tatizo kwangu, kwa sababu unaingia kwenye
mzozo wakati mashindano tayari yameshaanza na ninahitaji kuelekeza nguvu katika
mashindano.
“Si
rahisi tena kwa sababu soko la kimataifa lipo wazi zaidi. Kuna washindani wengi
lakini wachezaji ni wachache. Mara zote ninahitaji kuwa katika nafasi ambayo
sina wakununua. Ndiyo maana nina watu wanaonizunguka kunisaidia, lakini uamuzi
wa mwisho lazima hutokea kwa kocha.”
No comments:
Post a Comment