Manchester,
England
KOCHA
mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini anaamini kuwa, kwa mara ya kwanza
atafanikiwa kuivusha timu hiyo kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Kwa
misimu miwili iliyopita, City imeshindwa kuvuka hatua ya makundi licha ya
kutumia kitita kikubwa katika usajili.
Hata
hivyo, katika michuano ya msimu huu hatua ya makundi, licha ya kupanga pamoja
na bingwa mtetezi Bayern Munich, pamoja na CSKA Moscow na Viktoria Plzen ya
Czech, Pellegrini amejigamba kuivusha miamba hiyo ya Etihad.
Akijivunia
historia yake ya msimu uliopita ya kuivusha Malaga hatua ya mtoano, Pellegrini
alisema: "Labda timu moja inaweza kuwa na historia kuliko nyingine kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini ninauhakika msimu uliopita wakati Milan ilipojua
kuwa ipo kundi moja na Malaga walifurahia kwa kuwa tulikuwa dhaifu, ila
tulijipanga na kisha kuvuka."
@@@@@@@@@
Mourinho:
Bado jembe moja
London: KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho licha ya kufanikiwa
kumsajili Samuel Eto'o kutoka Anzi, bado anahitaji mshambuliaji mmoja kabla ya
dirisha la usajili kufungwa leo usiku.
Taarifa
zimeeleza kuwa, Mourinho anataka kurejea maombi yake aliyoyatoa kwa
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Robert Lewandowski wakati akiwa Real Madrid,
sambamba na kujaribu bahati kwa Karim Benzema.
@@@@@@@@@
Tevez
azidi kuinogesha Juventus
Milan:
MSHAMBULIAJI mpya wa Juventus, Carlos
Tevez amefunga mechi tatu mfululizo alizocheza Serie A, ambapo juzi
alikamilisha idadi hiyo kwa kucheka na nyavu mara moja, wakati mabingwa hao wa Italia wakiibuka na ushindi
wa mabao 4-1 dhidi ya Lazio.
Arturo
Vidal ndiye aliyefunga mabao mawili ya awali, huku Miroslav Klose akifanikiwa
kupunguza idadi hiyo ya mabao kwa upande wa Lazio, kabla ya Mirko Vucinic
kutupia la tatu huku Tevez akihitimisha ushindi huo kwa kufunga la nne.
No comments:
Post a Comment