Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, September 16, 2013

OZIL ALIFUNIKA WAGENI MECHI YA KWANZA



MWISHO wa wiki hii wachezaji wengi waliosajili kwenye dakika za mwisho za dirisha la usajili la majira ya Kiangazi walipata nafasi ya kucheza mechi zao za kwanza. Bingwa linaangalia kilichofanywa na wachezaji hao kwenye Ligi Kuu England ‘wikiendi’ hii.

Marouane Fellaini (Manchester United)
Thamani: Pauni milioni 27.5 (Sh bilioni 68.759)
Dakika uwanjani: 28
Matokeo: Man United 2-0 Crystal Palace
Maksi: 6/10
Alichofanya
Fellaini aliingia uwanjani katika kipindi cha pili cha mchezo ambao Man United walionekana kuutawala dhidi ya wachezaji 10 wa Palace. Alifiti moja kwa moja kwenye kiungo cha kati ya timu hiyo, hakukosea na akiwa uwanjani Man United walipata bao lao la pili.
Mbelgiji huyo alichukua nafasi ya Anderson, ambaye alionekana kuchemka uwanjani, huku mashabiki wa Man United wakiomba Fellaini aingie, na kuna kila dalili kwamba ataanza kwenye mechi dhidi ya Manchester City wiki ijayo.

Mesut Ozil (Arsenal)
Thamani: Pauni milioni 42.5 (sh bilioni 106.265)
Dakika uwanjani: 80
Matokeo: Arsenal 3-1 Sunderland
Maksi: 9/10
Alichofanya
Kama ilivyotarajiwa na wengi alifanya vizuri. Kiungo huyo mchezeshaji alitengeneza bao moja na kuhakikisha kwamba Arsenal hawalioni pengo la majeruhi Santi Cazorla na alimtengenezea Theo Walcott nafasi mbili za wazi, lakini Muingereza huyo alishindwa kufunga. Ozil alitolewa uwanjani zikiwa zimesalia dakika 10 mpira kwisha, mashabiki wote walisimama na kumpigia makofi, Ozil anatabiriwa kuwa moto zaidi msimu ujao.

Christian Eriksen (Tottenham)
Thamani: Pauni milioni 11.5 (Sh bilioni 28.754)
Dakika uwanjani: 71
Matokeo: Tottenham 2-0 Norwich
Maksi: 8/10
Alichofanya
Christian Eriksen ambaye amesajiliwa kutoka Ajax ni kiungo mshambuliaji mbunifu sana na alithibitisha hilo Jumamosi, kutokana na kumpigia pasi maridadi ya mwisho Gylfi Sigurdsson ambaye alifunga bao la kwanza kwenye mechi hiyo.
Japokuwa atakuja kuchukua namba ya Sigurdsson, pale mastaa Aaron Lennon na Erik Lamela watakapokuwa fiti kuanza, juzi alimtengenezea nafasi za kufunga, alionyesha kiwango kikubwa mpaka anatolewa katika dakika ya 71.

Samuel Eto'o (Chelsea)
Thamani: Bure
Dakika uwanjani: 90
Matokeo: Everton 1-0 Chelsea
Maksi: 6/10
Alichofanya
Eto'o alitengenezewa nafasi kadhaa za kufunga, lakini alikosa zote. Ya kwanza ilionekana kabisa kama ni bao, ila Gareth Barry aliwahi na kuzuia shuti lake ambalo lilikuwa likielekea golini ambako hakukuwa na mtu, aligongesha mwamba baada ya kupiga kichwa krosi iliyopigwa na Ramires. Anaweza kujitetea kwamba bado hajawa fiti kucheza mechi za kiushindani.

Gareth Barry (Everton)
Thamani: Mkopo
Dakika uwanjani: 90
Matokeo: Everton 1-0 Chelsea
Maksi: 8/10
Alichofanya
Alikuwa na mechi nzuri kwenye eneo la kiungo. Akicheza sambamba na Ross Barkley walishirikiana kuivunjavunja Chelsea na kitu mihumu kuliko chote alichokifanya ni kuzuia shuti la Eto’o ambalo lilikuwa linaenda golini, na kumnyima Mcameroon huyo bao la wazi.

Loic Remy (Newcastle)
Thamani: Mkopo
Dakika uwanjani: 63
Matokeo: Aston Villa 1-2 Newcastle
Maksi: 6/10
Alichofanya
Hakuonyesha kiwango cha kutisha sana kwenye mechi hiyo na kujikuta akitolewa uwanjani katika dakika ya 63. Staa wa Newcastle kwenye mechi hiyo alikuwa Hatem Ben Arfa, kama timu hiyo inataka kufanya vizuri basi wanahitaji mabao kutoka kwa Papiss Cisse au Remy.

Stevan Jovetic (Man City)
Thamani: Pauni milioni 22 (Sh bilioni 55)
Dakika uwanjani: 63
Matokeo: Stoke 0-0 Man City
Maksi: 5/10
Alichofanya
Japokuwa hakusajili kwenye siku ya mwisho ya dirisha la usajili, mechi hii ndiyo ilikuwa ya kwanza ya kimashindano kwake, na hakuonyesha kiwango kizuri.
Alijaribu kuonyesha thamani yake, lakini mabeki wa Stoke walimzuia asilete madhara na alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Sergio Aguero. Atafanya vizuri siku za usoni, lakini mechi ya juzi hakuwa yake kabisa.

Marko Arnautovic (Stoke)
Thamani: Pauni milioni 2 (Sh bilioni 5)
Dakika uwanjani: 20
Matokeo: Stoke 0-0 Man City
Maksi: 7/10
Alichofanya
Marko Arnautovic anajulikana kwa jina la utani la the Austrian Balotelli (Balotelli wa Austria), lakini jamaa huyo hakuonyesha utata mwingi kwenye mechi dhidi ya Man City.
Alikaribia kufunga bao kwenye shuti la mwisho la mechi, alipiga shuti ambalo lililopaa kidogo juu ya lango. Kabla ya hapo alikaribia kulazimisha bao la kujifunga la Matija Nastasic.

Victor Anichebe (West Brom)
Thamani: Pauni milioni 6 (Sh bilioni 15)
Dakika uwanjani: 78
Matokeo: Fulham 1-1 West Brom
Maksi: 6/10
Alichofanya
Alicheza vizuri mbele akiwa mwenyewe, lakini umaliziaji wake ulikuwa mbovu. Anichebe alishindwa kuvuma akiwa Everton, japokuwa alipewa nafasi ya kuvuma, inawezekana akachemka na West Brom pia. Alicheza kiwango kizuri, lakini hakuwa na jipya.


No comments:

Post a Comment