Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Eliud Mvella amejiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika
Oktoba 27 mwaka huu.
Mvella
amemwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu
Mbwezeleni akielezea uamuzi wake huo pamoja na mambo mengine umetokana
na kile alichodai kuwa Kamati hiyo haikumtendea haki kwa kumwondoa.
Mbwezeleni
amekiri kupokea barua hiyo, na kuongeza kuwa licha ya uamuzi huo wa
Mvella aliyekuwa ameomba kuwania ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia
Kanda Namba Saba ya mikoa ya Iringa na Mbeya, bado suala lake
litasikilizwa na Kamati ya Maadili ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi.
Kamati
ya Mbwezeleni ilimuondoa Mvella katika kinyang’anyiro hicho kwa
kushindwa kuheshimu Kanuni za Uwajibikaji wa Pamoja (collective
responsibility) baada ya kushiriki kufanya uamuzi ndani ya Kamati ya
Utendaji ya TFF bila ya kutaka msimamo wake wa kupinga uwekwe kwenye
muhtasari na baadaye kuupinga uamuzi huo akiwa kwenye uongozi wa mkoa.
No comments:
Post a Comment