KOCHA WA IRELAND TRAPATTONI ABWAGA MANYANGA BAADA YA KICHAPO CHA AUSTRIA
Meneja Giovanni Trapattoni ameondoka
katika kazi yake ya kuifundisha Jamhuri ya Ireland kufuatia mazungumzo
baina yake na chama cha soka cha nchi hiyo baada ya kichapo cha Austria
ukiwa ni mchezo wa kuwani kufuzu kombe la dunia.
Chama cha soka cha Ireland kimetangaza kuondoka kwa meneja huyo hii
leo baada ya kukutana na Trapattoni na msaidizi wake Marco Tardelli.
Wawili hao walikuwa na mkataba na chama hicho mpaka mwishoni mwa mwezi Mei 2014.
Akiwa kazini kwa miaka miatano, Trapattoni aliiongoza Ireland kufikia fainali ya Euro 2012.
Trapattoni's Ireland record
Matches: 64
Wins: 26
Draws: 22
Defeats 16
Kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Austria kumeiiacha Ireland katika
hali mbali kimahesabu na kuifanya Sweden kushika nafasi ya pili katika
kundi C.
Muda mfupi baada ya mchezo uliopigwa Vienna hapo jana, meneja huyo
mwenye umri wa miaka 74 alisikika akisema anasubiri maamuzi ya FAI
kuamua juu ya hatma yake ya baadaye.
No comments:
Post a Comment