Mkurugenzi
wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Sunday Kayuni
atashiriki warsha ya wakufunzi wa makocha wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) itakayofanyika kuanzia Oktoba 22-24 mwaka huu.
Warsha
hiyo iliyoandaliwa na CAF kwa ajili ya wakufunzi wake itafanyika nchini
Cameroon. Wakufunzi 18 wa CAF kwa upande wa makocha watahudhuria warsha hiyo.
Madhumuni
ya warsha hiyo ni kuainisha majukumu yao, kubadilishana uzoefu. Pia kuwapa
methodolojia mpya ya ufundishaji na muongozo kuhusu mfumo wa leseni za makocha
ambao watautumia katika nchi wanazotoka.
Mbali
ya Kayuni Tanzania, wakufunzi wengine ni Ahmed Babiker (Sudan), Amadou Shaibu
(Nigeria), Boy Bizzah Mkhonta (Swaziland), Duodu Fred Osam (Ghana), Edussei
Anthony (Ghana), Fathi Nossir (Misri), Faouzy Altaisha (Sudan) na Fran Hilton
Smith (Afrika Kusini).
Wengine
ni Francis Oti-Akenteng (Ghana), Honour Janza (Zambia), Kasimawo Laloko
(Nigeria), Mahmoud Saad (Misri), Paul Hamilton (Nigeria), Serame Letsoaka
(Afrika Kusini), Shawky Abdel Shafy (Misri), Thondoo Govinder (Mauritius) na
Ulric Mathiot (Seychelles),
No comments:
Post a Comment