MADRID, Hispania
LICHA ya ndoto za mshambuliaji,
Gareth Bale kukipiga Real Madrid
kukamilika usiku wa kuamikia jana, bado
kuna wingu zito kuhusu bei aliyonunuliwa mchezaji huyo, baada ya kila
upande kutangaza bei tofauti.
Kwa mujibu wa gazeti la Sport Star,
mkanganyiko kuhusu bei aliyonunuliwa nyota huyo, ambaye alitarajiwa
kutambulishwa jana baada ya kufuzu vipimo vya afya, uliibuka baada ya Tottenham
kudai kuwa imemuuza kwa bei iliyovunja rekodi ya usajili duniani ya pauni milioni 85.2, huku Real Madrid ikisisitiza kuwa haijamnunua Bale kwa
bei hiyo, bali fedha iliyoitoa ni pauni milioni 78, kiasi ambacho ni pauni
milioni 2 chini ya zile ilizoilipa, Manchester United ili imuachie Cristiano Ronaldo miaka minne iliyopita.
Mvutano umeacha maswali mengi kwa
wadau wa soka ulimwenguni, wakihoji kuwa nani mkweli kuhusu usajili huo ama
kuna kitu gani kilichofichwa nyuma ya pazia la usajili huo.
Vyanzo vingine vya habari vinadai Bale ambaye amesaini mkataba wa miaka sita
kuichezea miamba hiyo ya Santiago Bernabeu, atakuwa akiingiza kiasi cha pauni
300,000 kwa wiki na kuwa miongoni mwa wacheza soka watakaokuwa wakilipwa zaidi
duniani.
Kwa ujumla inasemekana Madrid wametumia jumla ya
kiasi cha pauni milioni 176 kumsajili staa huyo wa Wales, ambapo pauni milioni
86 ni usajili na pauni milioni 90 ni mshahara wake.
Bale bado hajamfikia Lionel Messi ambaye ndiye
mchezaji anayelipwa zaidi kwa sasa duniani akiingiza kiasi cha pauni milioni
27.4, kutokana na mshahara, marupurupu na mikataba ya kibiashara mwaka jana
pekee.
Cristiano Ronaldo (28), anaingiza pauni milioni 24,
mwaka jana pia, wakati mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney (27)
ndiye mchezaji anayelipwa zaidi Ligi Kuu England, anaingiza pauni milioni 17
kwa mwaka.
Wakati timu hizo zikivutana kuhusu
bei hiyo, kwa upande wake Bale ambaye amesaini mkataba wa miaka sita kuitumikia
klabu hiyo, akizungumzia kuhusu usajili huo alisema: "Nafahamu wachezaji
wengi mara nyingi huwa wakizungumzia kuhusu
kuwa na ndoto za kuchezea timu walipokulia, lakini kwangu mimi kwa kuwa mkweli
ndoto yangu imekuwa kweli.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
Mtendaji wa Tottenham, Daniel Levy, alisema kuwa hakuweza kuweka kingingi
kumruhusu Bale, akisema kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 asingeweza kujituma endapo wangemlazimisha
kubaki.
Baada ya kukamilika usajili huo, Bale
atashuka uwanjani kuikabili Villarreal Jumamosi ijayo, katika mechi ya Ligi Kuu ya
Hispania, La Liga.
Real
Madrid wamevunja Rekodi ya Dunia kwa Ada ya Uhamisho kwa kuilipa Tottenham
PauniMilioni 85 kumnunua Gareth Bale na kukamilisha Uhamisho wake.
Mwaka
2009, Real Madrid waliweka Rekodi kwa kumnunua Cristiano Ronaldo kutoka
Manchester United kwa Pauni Milioni 80 na jana wamekamilisha Uhamisho wa Bale na
kuivunja Rekodi yao wenyewe.
Baada ya Dili hii kukamilika na kutangazwa rasmi, Bale, Miaka 24 ambaye ni Raia wa Wales, alitamka: “Nilikuwa na Miaka 6 ya furaha pale Tottenham na sasa ni wakati kusema Kwaheri!”
Leo, Bale amepimwa afya yake huko Madrid na kuonyeshwa kwa Mashabiki wa Real Madrid Saa 8 Mchana kwa Saa za Bongo.
Bale alijiunga na Tottenham kama Fulbeki wa kushoto kutoka Southampton Mwaka 2007 kwa Pauni Milioni 10 na Msimu uliopita kufunga Bao 26 na pia kutwaa Tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Mwaka, za PFA na FWA.
Bale anakuwa Mchezaji watano kusainiwa na Real Madrid katika Kipindi hiki cha Uhamisho.
Kukamilika kwa Dili hii ya Bale kunamaliza Uhamisho uliokuwa ni vuta nikuvute ya muda mrefu na kutawala Vichwa vya Habari Dunia nzima.

No comments:
Post a Comment