Mathieu Flamini enzi hizo.
Aliichezea Arsenal zaidi ya michezo 100 , Flamini aliihama Arsenal na kujunga na AC Milan mwaka 2008
Siku
12 za marekebisho ya kikosi cha Arsene Wenger zinaonekana kuelekea
pazuri kwani taarifa zinasena kuwa Arsenal huenda ikapata mkataba na
Mathieu
Flamini, ikiwa ni miaka mitano baada ya mchezaji huyo kuihama klabu hiyo
na kujiunga na AC Milan.
Milan ilimuacha kiungo huyo mwenye umri
wa miaka 29 mwishoni mwa msimu na tangu wakati huo amekuwa akifanya
mazoezi na kikosi cha Wenger katika kipindi cha wiki mbili sasa.
Meneja wa Arsenal amekuwa akivutiwa na
Flamini na anataka kumpa mkataba ambapo inaarifiwa kuwa Flamini licha ya
kuwepo na hali ya kutakiwa na vilabu vingine.
Huo utakuwa ni usajili wa pili kwa
Wenger ambapo utakuwa ni usajili wa pili huru na usajili wa wanne kwa
wachezaji wake wa zamani kurejea kikosini kwani alikwisha kufanya hivyo
huko kwa akina Sol Campbell, Jens Lehmann na
Thierry Henry (mara mbili) ambao walirejea Emirates.
Usajili wa Flamini huenda ukakamilishwa kesho na huenda akawepo dimbani katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Fulham.
Arsenal old-boy: Thierry Henry
alitangazwa kurejea wakati mwaka 2012 ambapo alifunga goli klatika
michuano ya FA dhidi ya Leeds i2012.
Jens Lehmann na Sol Campbell pia walirejea kwa Arsene Wenger baada ya kuwa uhamishoni London ya kaskazini.
Flamini alijiunga na kikosi hicho cha
Italia cha Milan lakini alisumbuliwa na hali ya ubora wa afya yake ikiwa
ni pamoja na kupatwa na matatizo ya mguu matatizo ambayo yalimuweka n
je ya uwanja kwa msimu mzima wa 2011-12.
Wenger
anaimani kuwa kurejea kwa Flamini kutarejesha uzoefu baada ya kukabiliw na majeruhi na wengine kadhaa kuondoka kikosini.
Viungo Mikel Arteta, Abou Diaby na Alex Oxlade-Chamberlain wote ni majeruhi.
Flamini kutoka San Siro narejea tena Arsenal.
Laurent Koscielny jana alijeruhiwa
No comments:
Post a Comment