Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, August 11, 2013

SURE BOY ATAKIWA APATA ULAJI SAUZI, KUUZWA KWA OLRANDO PIRATES DOLA 300,000


NA ONESMO KAPINGA, JOHANNESBURG
KIUNGO wa Azam FC, Sulum Abubakari  'Sureboy', anatakiwa na Klabu ya Olrando Pirates kwa dau la dola 300,000 za Kimarekani, sawa na zaidi ya Sh. Milioni 400 za Tanzania.
Klabu ya Orlando imeonyesha nia ya kumsajili baada ya kuvutiwa na kiwango chake alichokionyesha katika mechi tatu za kirafiki za kimataifa ambazo Azam FC ilicheza jijini hapa.

Sureboy, ambaye ni kiungo cha timu ya Taifa 'Taifa Stars', alikuwa akifuatiliwa kwa karibu na mawakala ambao walikuwa wanafika kwenye mechi za kirafiki za kimataifa ambazo Azam FC imekuwa ikicheza hapa.
Uongozi wa Klabu ya Olrando Pirates umevutiwa na Sureboy baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika mechi ya  kwanza dhidi ya Kaizer Chiefs, ambapo Azam ilifungwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Kaizer Chiefs Sports Village, uliopo eneo la Naturena.

Azam  FC ilishinda mchezo wa pili kwa bao 1-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns, kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo, ambapo Sureboy alionyesha uwezo mkubwa huku akiwavutia mawakala wengi.
Katika mechi dhidi ya Olrando iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Randstadium na Azam FC kufungwa mabao 2-1, baada ya kumalizika uongozi wa klabu hiyo iliwafuata viongozi wa Azam FC na kufanya mazungumzo ya kumtaka Sureboy.

Akizungumza jijini hapa, Meneja wa Azam FC,  Said Jemedari, alisema viongozi wa Olrando waliwafuata kwa lengo la kumtaka Sureboy kufanya majaribio kwenye klabu yao, kutokana na kuridhika na kiwango chake.

Jemedari alisema klabu hiyo inaweza kumkosa Sureboy kwa sababu msimu wa usajili umemalizika na wao kama Azam hawataweza kumpata mchezaji mwingine kwa sasa kufidia pengo la Sureboy, iwapo watamuuza.

Wakati  huo huo, Sureboy ameumia  baada ya kujitokeza uvimbe wa nyama katika mechi yao dhidi ya Olrando Pirates.
Kwa mujibu wa Daktari wa timu hiyo, Vicent Madege, kutokana na tatizo lake, atalazimika kukaa nje kwa muda wa siku tatu akipatiwa matibabu.



No comments:

Post a Comment