Leo usiku huko Estadio Vicente Calderon, Atletico Madrid itawakaribisha Barcelona kwenye Mechi ya kwanza ya Supercopa De Espana Kombe ambalo hushindaniwa mwanzoni mwa Msimu kati ya Bingwa wa La Liga, ambae ni Barcelona, na Bingwa wa Copa Del Rey, ambae ni Atletico Madrid.
Lakini wakati Mechi hii ikingojewa kwa hamu, huku baadhi wakitaka kumuona aliekuwa Straika wa Barcelona, David Villa, akiichezea Atletico Madrid kwa mara ya kwanza dhidi ya Barca tangu ahamie hapo Mwezi uliopita.
Jumapili Barcelona wallianza utetezi wao wa La Liga chini ya Meneja mpya Gerardo ‘Tata’ Martino kwa kishindo walipoitwanga Levante Bao 7-0 Uwanjani Nou Camp.
Atletico Madrid nao walianza Msimu wao mpya wa La Liga kwa ushindi wa Ugenini wa Bao 3-1 walipocheza na Sevilla huku Diego Costa, Mchezaji kutoka Brazil, akiwafungia Bao 2 na kuonyesha kuwa anao uwezo wa kuziba pengo lililoachwa na Straika wa Colombia, Radamel Falcao, alieihama Atletico na kwenda Monaco.
Akizungumzia Soka la Spain, Kocha wa Atletico ambae alikuwa Kiungo wa zamani wa Argentina, Diego Simeone, ameonyesha kukata tamaa na jinsi Vigogo Barca na Real Madrid wanavyotawala Soka la Spain.
Simeone ametamka: “Real na Barca wapo Ligi nyingine. Haya ni Mashindano yaliyopooza kwa Wadau wengine ambao wanashindania kuchukua Nafasi za 3 au za 4 tu. Inabidi tusubiri njia nyingine ya Mgao wa Fedha za TV kwa sababu kwa sasa Ligi hii ni ya Wawili tu!”
Barcelona na Atletico Madrid zitacheza Mechi ya Marudiano ya Supercopa De Espana hapo Jumatano Agosti 28 huko Uwanja wa Nou Camp.
No comments:
Post a Comment