UONGOZI wa Boom FC umelishukuru Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF), kwa kuipatia msaada wa Sh 5,125,000 kwa ajili ya uendeshaji wa
timu hiyo katika Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu mkuu wa Boom
FC, Duni Mibavu amesema fedha hizo zitasaidia timu kufanya vizuri katika ligi
na kuwapa morali wachezaji ili kuhakikisha timu hiyo inacheza Ligi Daraja la
Kwanza msimu ujao.
“Tunawashukuru wenzetu wa NSSF chini ya Mkurugenzi wake Dk.
Ramadhan Dau kwa msaada mkubwa walioutupatia, hii inaonyesha ni jinsi gani
walivyoguswa na na kilio chetu na kuamua kutusaidia ili tufanye vizuri,”
alisema.
Duni ameomba na mashirika mengine pamoja na makampuni
mbalimbali nayo kuiga mfano wa NSSF katika kuzisaidia timu za madaraja ya chini
ili nazo zifanye vizuri.
No comments:
Post a Comment