Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 12, 2013

KOCHA BRENDAN RODGERS ASISITIZA TENA KUWA SUAREZ HAONDOKI

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers anaamini kuwa klabu hiyo bado imedhibiti mustakali wa Luis Suarez na kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay atarejea katika kiwango chake cha msimu uliopita mara atakapogundua kuwa hataruhusiwa kuondoka. Arsenal wameendelea kumnyatia Suarez ambaye msimu uliopita ndiye alikuwa mfungaji wa kutegemewa wa Liverpool, kwa kutaka kuongeza ofa zaidi baada ya ile ya paundi milioni 40 kukataliwa.  Mapema jana Wenger alithibitisha kuwa anategemea kusajili mshambuliaji huyo lakini Rodgers ambaye alimlazimisha mchezaji huyo kufanya mazoezi mwenyewe kufuatia kauli yake ya kutaka kuondoka aliyoitoa, bado ana imani Suarez atabakia Anfield. Rodgers amesema hana shaka kwamba mchezaji huyo atabakia hapo kwasababu bado ana mkataba na Liverpool na pindi atakapogundua hilo anadhani ataanza kujituma kama ilivyokuwa msimu uliopita. 

No comments:

Post a Comment