Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 12, 2013

DAVID MOYES: 'NGAO YA JAMII NI TAJI JINGINE KWA FERGIE!', AKANUSHA BIFU NA ROONEY, ASISITIZA HAUZWI!! AMKOSHA MZEE FERG

MARA baada ya kutwaa Taji lake la kwanza baada ya Jana kuifunga Wigan Athletics Bao 2-0 na kutwaa Ngao ya Jamii, Meneja wa Manchester United, David Moyes amekanusha kuwepo na kutoelewana na Wayne Rooney na pia kusisitiza Mchezaji huyo hauzwi. 

Pia, Moyes alitoboa kuwa wanakaribia kusaini Wachezaji wapya. 
Akihojiwa mara baada kuifunga Wigan 2-0 Uwanjani Wembley, Moyes aliulizwa inakuwaje Rooney hakuweza kucheza kwennye Mechi hiyo ya Ngao ya Jamii lakini atacheza Jumatano wakati England inacheza Mechi ya Kirafiki na Scotland Uwanjani Wembley, alitania: “Sioni kwa nini hilo linakuchanganya. Ni Gemu kubwa kwa Scotland! Unadhani nitampeleka Mchezaji fiti acheze na Scotland?”

David Moyes ni Mtu wa asili ya Scotland na baada ya kuacha utani akafafanua: “Nimeshaongea na Roy Hodgson. Rooney amefanya mazoezi na pengine wengine hampendi kusikia hili, sina ugomvi na Rooney! Wengine huwa mnaandika ‘nusu ukweli!’ Huwa mnawahadaa Wasomaji wenu!” Winners: Manchester United's Nemanja Vidic raises the Community Shield after his side's 2-0 victory
Washindi  Manchester United wakiwa wanafuraha hapa na mchezaji  Nemanja Vidic akiwa amelibeba kombe hilo juu kombe la  Ngao ya Jamii baada ya timu kuibuka kidedea jioni hii.
Here to spray: Manchester United's players celebrate their success in the season's tradition curtain-raiser
Wachezaji wa Manchester United wakifurahia ushindi kwa kupata kombe hilo na kuanza nalo msimu mpyaMtanikomaa....Endelea nalo kijana...waoneshe!!!
Baada ya kusisitiza kuwa Rooney hauzwi licha ya kuwepo kwa habari kuwa Chelsea wanataka kuja na Ofa ya tatu baada ya mbili za kwanza, £20m na £25m, kukataliwa, Moyes alisema: “Ninataka ajiunge na England. Alifanya Mazoezi na Kikosi cha Kwanza Jumamosi. Hayupo tayari kwa Mechi na pengine mtaona hilo Jumatano. Pengine atacheza sehemu ya Gemu hiyo lakini hajacheza Mechi yeyote mbali ya Dakika 45 alizocheza na Real Betis Mechi ya Kirafiki na kuumia Bega. Haiwezekani kwa hali hiyo acheze Mechi, hakuwa tayari leo lakini pengine Jumatano atacheza.”

Kuhusu Wachezaji wapya, Moyes alisema: “Tunakaribia kusaini wapya. Tumepiga hatua kwa hilo. Lakini ikiwa hatutasaini mpya basi hata hawa niliokuwa nao wanafaa sana!”
MOYES: ‘NI TAJI JINGINE KWA FERGIE!’
Jana, mara baada ya Timu yake kutwaa Ngao ya Jamii, David Moyes amesema Taji hilo ni la Meneja aliemrithi hapo Manchester United, Sir Alex Ferguson. 

Sir Alex Ferguson aliamua kustaafu Mwezi Mei baada ya kutwaa Vikombe 38 katika Miaka yake 26 huko Old Trafford.

Moyes ametamka: “Hili ni Taji jingine kwa Sir Alex Ferguson! Leo nimeongoza Timu lakini hii ni zawadi kwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England chini ya Sir Alex Msimu uliopita!” 


No comments:

Post a Comment