AMISSI TAMBWE NA GILBERT KAZE WAPATA HATI ZA UHAMISHO WA KIMATAIFA (ICT)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MWENYEKITI wa Simba, Mhe; Ismail Aden Rage, leo mchana amefanikisha
upatikanaji wa Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC), kwa wachezaji wawili
wa klabu hiyo kutoka nchini Burundi -Amissi Tambwe na Gilbert Kaze.
Wachezaji hao wawili ambao pia ni tegemeo la timu ya soka ya taifa ya
Burundi (Intamba Murugamba), hawakucheza katika mechi ya Ligi Kuu ya
Tanzania iliyochezwa jana kutokana na kutokamlika kwa uhamisho huo,
jambo lililoleta usumbufu mkubwa kwa benchi la ufundi, wachezaji
wenyewe, uongozi na wapenzi na washabiki wa klabu.
Rage
aliondoka jijini Dar es Salaam jana usiku na imechukua chini ya saa 24
kuweka kufanikisha suala hilo. Katika taarifa yake kwa wana Simba,
Mbunge huyo wa Tabora Mjini alisema amelazimika kuingilia kati suala
hilo kwa sababu lilihusu baadhi ya taratibu muhimu za Shirikisho la Soka
Duniani (FIFA) na ukweli kwamba viongozi wa Vital O, klabu waliyotoka
wachezaji hao hawakuwa mjni na hivyo kuchelewa kwao kungeigharimu Simba.
"Kila walipokuwa wakipigiwa simu kwa takribani siku tatu mfululizo
walikuwa wakisema kwamba wako milimani. Sasa hawa watu wa Burundi
wakikwambia wako miliman wanamaanisha wameenda kijijini kwao. Kuongea
kwa simu pekee kusingetosha na ndiyo Kamati ya Utendaji ya Simba iliomba
niende mwenyewe Burundi ili suala hili liishe," alisema.
Hii
ni mara ya pili kwa Rage, ambaye ana uzoefu wa kuongoza soka kwa zaidi
ya miongo mitatu, kuingilia kati suala la uhamisho wa wachezaji wa
kimataifa. Miaka miwili iliyopita, Mwenyekiti huyo alilazimika pia
kusafiri kwenda nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kushughulikia uhamisho
wa mchezaji Gervais Kago ambao nao ulikuwa na matatizo.
Kutokana na kupatikana kwa ITC hizo, Kaze na Tambwe sasa wataruhusiwa
kucheza katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya JKT OIljoro ya Arusha
iliyopangwa kufanyika Jumatano ijayo mjini Arusha. Klabu ya Simba tayari
imewakatia wachezaji hao vibali vya kufanya kazi hapa nchini.
Wachezaji wengine wa kigeni wa Simba, Joeph Owino na Abel Dhaira,
walicheza katika mechi ya jana kutokana na kukamilisha taratibu zote za
uhamisho na kuwa na vibali vya kufanya kazi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment