MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rafael M.
Muhuga, amesema JKT inajivunia kuibua vipaji vya michezo mbalimbali na
kuendeleza pia kuwa na timu zenye ushindani mkubwa kwenye soka la Tanzania.
Muhuga aliyasema hayo jana wakati akifungua mashindano ya
kuadhimisha miaka 50 ya Jeshi la Kujenga Taifa kwenye Uwanja wa Karume uliopo
Ilala jijini Dar es Salaam nakuwataka wachezaji wanaoshiriki mashindano
wacheze kwa kufuata taratibu kuepuka
kuumiza.
Pia alisema kauli mbiu ya mashindano hayo ni ‘Tunajivunia malezi bora ya vijana,
uzalishaji mali, Ulinzi na linasonga mbele’ na ndio maana serikali imeamua
kurudisha JKT kwa vijana ili wapate malezi borana kuzalisha mali huku
wakiendekleza pia ulinzi wa nchi.
Mashindano hayo yanashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo
mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa pete, wavu, mpira wa mikono, ngoma na michezo mingine yote.
Kwenye mchezo wa ufunguzi timu ya JKT Ruvu inayoshiriki ligi
kuu ya Tanzania bara ilishindwa kutamba mbele ya JKT Kanembwa inayoshiriki ligi
daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana.
Hata hivyo washambuliaji wa JKT Ruvu wakiongozwa na Musa Mgosi walikosa mabao ya wazi mara kadhaa kwenye
kipindi cha kwanza huku beki wao Stanley Nkomola akifanya kazi ya ziada kumkaba
Mfaume Peter kiungo mshambualiaji wa JKT Kanembwa kutokana na kuliandama lango
lao.
Mchezo mwingine ulizikutanisha JKT Oljoro na Ruvu Shooting
kwenye Uwanja wa Bandari, Kurasini ambapo JKT Oljoro ilishinda kwa bao 1-0.
Timu za soka zinazoshiriki mashindano hayo ni JKT Oljoro,
JKT Mgambo, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, JKU ya Zanzibar, JKT Mlale na JKT
Kanembwa.
No comments:
Post a Comment