LONDON,
England
TIMU
ya Tottenham imewafanyia kitu kibaya mahasimu wao jijini London, timu za
Arsenal na Chelsea, baada ya kuzizidi maarifa na kufanikiwa kuwanasa makinda
wawili kutoka nchini Croatia.
Klabu hizo mbili za Chelsea na
Arsenal zilikuwa zikiwawania makinda wa timu ya Dinamo Zagreb, Alen
Halilovic na Tin Jedvaj, wote wakiwa na umri wa miaka 17.
Hata hivyo, Andre Villas-Boas ndiye
yupo mbioni kukubali kutoa kitita cha pauni milioni 17 ili kukamilisha usajili
wa makinda hao wawili.
Kiungo mshambuliaji Halilovic, msimu uliopita ndiye alikuwa
mchezaji wa pili kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na umri mdogo
na tayari ameshaonesha maajabu kwenye timu ya taifa ya Croatia ambayo
yanamfanya afananishwe na nyota wa zamani Spurs, Luka Modric.
Kwa upande wake, beki wa kati,
Jedvaj, yeye anakipiga kwenye timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka
19 na msimu uliopita ameichezea Dinamo mechi 13.
Rais wa Dinamo, Mirko Barisic,
alithibitisha usiku wa kuamkia jana kwamba makubaliano ya kuwasainisha nyota
hao wawili yameshakamilika.
@@@@@@@@@@@
Crouch: Nipo gizani
LONDON, England
MSHAMBULIAJI,
Peter Crouch, amesema kuwa hadi sasa yupo gizani kuhusu hatima ya kibarua chake katika timu ya Stoke City, chini ya kocha mpya, Mark Hughes.
Nyota huyo alijiunga na na timu hiyo
ya Britannia akitokea Tottenham misimu miwili iliyopita kwa
kitita cha pauni milioni 10 na ana makataba hadi mwaka 2015.
Hata hivyo, Crouch, mwenye umri wa
miaka 32, ambaye ameshachezea klabu 10
tofauti tangu aanze kusakata kandanda alisema jana: “Kutokana na historia yangu
huwezi kufahamu.
“Kamwe sijawahi kuwa na mawasiliano
ya mara kwa mara na Mark Hughes.
“Lakini nakumbuka nilimuona
akiwa Chelsea. Natarajia kufanya naye
kazi,” aliongeza nyota huyo.
No comments:
Post a Comment