RAIS wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga, amewataka makocha
kuhakikisha wanaibua vipaji vya watoto ili kuwa na vipaji vingi baadaye.
Tenga ametoa
rai hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo, wakati akifunga kozi
ya siku 21 ya makocha wa mchezo huo ngazi ya pili, iliyoandaliwa na Chama cha Mpira
wa Miguu Dar es Salaam (DRFA), huku ikishirikisha zaidi ya makocha 58.
Tenga
amesema Bara la Afrika ndilo bara lenye upungufu mkubwa wa wachezaji watoto,
tofauti na mabara mengine, kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya soka.
“Hili ndilo
bara ambalo lipo nyuma katika kuibua vipaji, mfano nchi ya Ujerumani pekee ina watoto
zaidi ya milioni moja ambao wanaandaliwa,
lakini hapa sijui kama wanafika hata idadi hiyo, hivyo kuna changamoto kubwa
katika hilo,” alisema.
Amewataka
kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo katika kuleta mabadiliko katika soka hapa
nchini, ambapo pia aliwapongeza kwa kushiriki katika kozi hiyo.
Naye
Mkurugenzi wa Ufundi wa DRFA, Joseph Kanakamfumu, alisema kozi hiyo imefanyika
kwa mafanikio makubwa, kwani walimu wote walikuwa wasikivu na wameweza kupata
mafunzo ya kutosha.
“Tunashukuru
Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA) kwa kuwezesha wakufunzi ambao waliweza
kuendesha mafunzo haya, lakini pia walimu hawa waliojitokeza tunawashukuru,”
alisema.
|
No comments:
Post a Comment