London,
England
JOSE
MOURINHO amewabwaga makocha wapya wenzake katika kura zilizopigwa kubashiri
kocha mwenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao.
Makocha
waliopigiwa kura ni Mourinho wa Chelsea, David Moyes wa Manchester United na
Manuel Pellegrini wa Manchester City ambao wamejiunga na klabu hizo majira haya
ya joto.
Mashabiki
wanaoaminika kwa upigaji kura za utabiri nchini England, walimpa Mounrinho
asilimia 52 ya kura 2,000 zilizopigwa.
Moyes
alipata kura 28, huku Kocha wa zamani wa Malaga, Pellegrini aliyetua City
akiambulia kura 14.
Kadhalika
mashabiki wengi walitabiri kuwa Mshambuliaji wa Kimataifa wa England, Wayne
Rooney, atakuwa bora zaidi endapo ataamua kubaki Manchester United
No comments:
Post a Comment