London,
England
KOCHA
wa Chelsea, Jose Mourinho anaamini kuwa wachezaji watano katika Kikosi chake cha
Stamford Bridge, ndiyo wenye uhakika wa kupata nafasi ya kuanza, jambo
linalomfanya amkubalie Arsene Wenger kumpigia kasi Mhispania, Fernando Torres.
Bosi
huyo wa Arsenal, Wenger anaitaka huduma ya Torres Emirates, wameripoti Dean
Jones na Dave Kidd wa Gazeti la The Sunday People.
Hata
hivyo, Mourinho yupo tayari kumruhusu Mhispania huyo kuondoka baada ya
kubainika kuwa katika mipango yake, hadi sasa wachezaji wenye uhakika wa kuanza
kwenye kikosi chake ni Petr Cech, Ashley Cole, Frank Lampard, Eden Hazard na
Oscar.
Mchezaji
mwenye Kipaji raia wa Hispania, Juan Mata na Beki wa Kati wa Kimataifa wa
Brazil, David Luiz pia si miongoni mwa watakaounda kikosi chake, hivyo watapewa
mkono wa kwaheri majira haya ya joto. Mourinho anaamini Oscar anastahili kucheza
namba 10, kutokana na kuwa bora kuliko Mata.
Lakini
hizo ni taarifa nzuri kwa Arsenal ambayo imejipanga kuelekea kwa Torres, ambaye
wanaamini ataweza kutengeneza kombinesheni nzuri Emirates akicheza sambamba na
Mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo Higuain wanayetarajia kumsajili.
Bodi
ya The Gunners ipo tayari kuona timu yao ikisajili nyota wengi, baada ya hivi
karibuni kushuhudia wachezaji wao wenye majina makubwa wakiihama klabu hiyo.
Torres,
ambaye yupo Brazil kwa majukumu ya kitaifa ambapo timu yake, Hispania jana
ilicheza mechi ya fainali ya Kombe la Mabara dhidi ya wenyeji hao, hana uhakika
kama yupo kwenye mipango ya baadaye ya Chelsea, hivyo anatarajia kuzungumza na
Mourinho wiki hii na Arsenal itampigia kasi 'fasta' kama atatemwa.
Chaguo
la kwanza kwa Arsenal ni Higuain, lakini Torres na Wayne Rooney wa Man United
pia wapo katika mipango yao.
Katika
hatua nyingine, Mourinho sasa atahitaji kusajili wachezaji sita kabla ya
dirisha la usajili kufungwa na anatambua wazi kuwa, pauni milioni 35 atakazozipata
kutokana na kumuuza Luiz kwa Barca, zitamtosha kuboresha kikosi chake.
Nyota
wa Brazil, Hulk anayeichezea Zenit St Petersburg, Mario Gomez wa Bayern Munich
na Mshambuliaji wa AC Milan, Stephan El Shaarawy wote wapo katika rada za
Mourinho, sambamba na Kifaa cha Manchester City, Edin Dzeko.
No comments:
Post a Comment