Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, June 30, 2013

DAVIS MOYES AKUTANA NA ROONEY KWA SIRI

 
Manchester, England

DAVID MOYES na Wayne Rooney wamekuwa na mkutano wa siri katika harakati za kocha huyo mpya wa Manchester United kutaka kuhakikisha anambakisha mshambuliaji huyo Old Trafford.

Msimu uliopita, Rooney alitibuana na Alex Ferguson, jambo lililomfanya aweke wazi dhamira yake ya kutaka kuondoka Old Trafford.

Taarifa za ndani zimeeleza: “Kuna hofu ndogo kwa kocha kutaka kumbakisha Wayne. Wamekutana kwa siri lakini nafasi kubwa imetolewa kwa Wayne kuamua mwenyewe kutoka moyoni.

“Mara zote amekua akitaka kuwekwa sokoni, hana furaha ya kutemwa katika mechi kubwa kama ile dhidi ya Real Madrid.”


Mshambuliaji huyo wa England, Rooney, 27, ambaye anawindwa na Arsenal, Chelsea, PSG na sasa Barcelona, anatarajiwa kukutana tena na Moyes wiki hii.

No comments:

Post a Comment