Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, June 30, 2013

REDNAPP AMPELEKA CESAR ARSENAL NA DAVID VILLA AKUBALI KUTUA SPURS

London:
KOCHA wa QPR, Harry Redknapp amethibitisha kuwa Julio Cesar ataihama klabu hiyo majira haya ya joto, wakati huu ambao Arsenal ikiaminika kuongoza katika mbio za kuipata huduma ya kipa huyo raia wa Brazil.

"Julio Cesar ataondoka," Redknapp alisema. "Ni kipa wa kiwango cha juu, namba moja wa Brazil. Amekuwa katika klabu kubwa na nyingi zinamhitaji kwa sasa, hataweza kucheza ligi daraja la kwanza (Championship)."


@@@@@@@@

David Villa akubali kutua Spurs

Barcelona: MSHAMBULIAJI wa Barcelona, David Villa, 31, wiki hii atatoa uamuzi wake endapo atatua Fiorentina ama Tottenham.

Hata hivyo, Villa ambaye jana alitarajiwa kuichezea Hispania dhidi ya Brazil kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Mabara, yupo tayari kutua Spurs badala ya Fiorentina na Barca inatarajia kuingiza pauni milioni 12 kama ada ya uhamisho.

No comments:

Post a Comment