SIMBA
imecheza rafu, baada ya kuzuia mikataba ya nyota watano wa Yanga, kwa ajili ya
msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Hatua
hiyo, inatokana na wachezaji hao ambao ni Frank Domayo, Simon Msuva, Kelvin
Yondani, Ally Mustapha ‘Barthez’ kuanza mazungumzo na viongozi wa Simba.
Wachezaji
hao ambao wamo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, inadaiwa
wamekataa kuendelea kuichezea Yanga pindi mikataba yao itakapomalizika.
Domayo
ambaye ni kiungo tegemezi katika Kikosi cha Yanga na Stars, alijiunga na timu
hiyo katika msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara akitokea JKT Ruvu na Msuva
Moro United, kisha kusaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja.
Kwa
upande wa Yondani na Barthez, walijiunga na timu hiyo wakitokea Simba katika msimu uliopita na kuiwezesha timu hiyo
kuchukua ubingwa wa ligi kuu.
Habari zilizopatikana kutoka ndani ya uongozi
wa Simba, zilieleza kwamba, wachezaji hao wameonyesha nia ya kutaka kuichezea
timu yao ya zamani, wakiamini wataweza kufikia malengo waliyojiwekea ya kucheza
soka katika klabu kubwa za Afrika na Ulaya.
Chanzo
hicho kilieleza kwamba, wanachosubiri wachezaji hao kwa sasa ni kumaliza
mikataba yao ili waweze kusaini Simba, hasa wakizingatia baadhi yao ni
wanachama hai wa klabu hiyo.
Kilieleza
kwamba, wachezaji hao wameona Simba ni klabu pekee inayoweza kuwauza na
wakacheza soka kwa mafanikio makubwa kama ilivyokuwa kwa wenzao, Mbwana Samatta
na Emmanuel Okwi.
Samatta
aliuzwa na Simba katika misimu mitatu iliyopita ya Ligi Kuu Tanzania Bara,
katika Klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya
kung’ara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho barani
Afrika, ambapo Okwi aliuzwa Etoile de Sahel ya Tunisia ambaye sasa anatarajiwa
kuuzwa Ulaya katika Klabu ya Partizan Beograd ya nchini Serbia.
Taarifa
zilizolifikia zilidai
kuwa Etoile de Sahel ipo katika mazungumzo na klabu hiyo ya Serbia, ambayo
inataka kumsajili Okwi baada ya kumvutia Kocha wao, Vuk Rasovic.
Partizan
Beograd imetwaa ubingwa wa Serbia msimu uliomalizika baada ya kumaliza ligi
hiyo inayoshirikisha timu 16 ikiwa na pointi 73, zikiwa ni pointi 11 mbele ya
Crvena Zvezda iliyomaliza ya pili na 12 dhidi ya Vojvodina Novi Sad ambayo
imeshika nafasi ya tatu.
Chanzo
hicho kilieleza kwamba, wachezaji wengi wanaounda kikosi cha kwanza cha Yanga
kama Mrisho Ngassa, Athumani Idd ‘Chuji’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Yondani na
Barthez na Kipa mpya wa timu hiyo, Deogratius Munishi ‘Dida’ ni wanachama hai
wa Klabu ya Simba
No comments:
Post a Comment