Nizar Khalfan (kulia) |
KIUNGO wa Yanga, Nizar Khalfan na beki wa timu hiyo, Oscar Joshua wameendelea kuula baada ya kuongezwa mikataba mipya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Shadrack Nsajigwa akitemwa kwenye kikosi hicho.
Msimu
uliopita Nsajigwa aliongezwa mkataba wa mwaka mmoja, baada ya kuichezea timu
hiyo kwa muda mrefu akitokea Moro United, hata hivyo, LENZI YA MICHEZO ina taarifa
kwamba anatarajiwa kupewa jukumu la kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.
Nsajigwa
wiki iliyopita alimaliza kozi ya ngazi ya pili ya ukocha iliyoandaliwa na Chama
cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), itakayomwezesha kukaa kwenye benchi la
ufundi la timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Habari zilizopatikana Dar es Salaam kutoka ndani
ya Kamati ya Usajili iliyochini ya Mwenyekiti wake, Abdallah Bin Kleb,
zilieleza Joshua na Nizar wameongezewa mkataba kwa kuwa bado wana mchango
mkubwa katika kikosi cha timu hiyo.
Chanzo
hicho kilieleza kwamba, wachezaji hao wameongezewa mkataba kutokana na
mapendekezo ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ernie Brandts, aliyeiwezesha Yanga
kuchukua ubingwa msimu uliopita.
“Wachezaji hao mikataba yao ilikuwa
imemalizika, tumeamua kuwaongezea ili waweze kuisaidia timu yetu katika msimu
ujao wa ligi kuu na Ligi ya Mabingwa mwakani,” kilieleza chanzo chetu.
Kilieleza
kwamba baadhi ya wachezaji akiwemo Stephano Mwasyika, Godfrey Taita, Said
Mohamed, hawajaongezewa kutokana na mikataba yao imemalizika huku wakionekana
si msaada tena kwa timu.
Wakati
huo huo, Brandts anatarajia kutua nchini leo
akitokea kwao Uholanzi alikokuwa kwenye mapumziko, baada ya kumalizika
kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga
ambao ni mabingwa wa ligi hiyo, wanatarajia kuanza mazoezi kesho kujiandaa na
msimu ujao.
No comments:
Post a Comment