Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Udalali ya Flamingo, Nyalila Noel akipandika hati ya mahakama katika basi la Shirikisho la soka Tanzania (TFF), ambayo inaruhusu kukamatwa kwa mali za shirikisho hilo.
Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Udalali ya Flamingo, Nyalila Noel akibandika hati ya mahakama katika basi la Shirikisho la soka Tanzania (TFF), ambayo inaruhusu kukamatwa kwa mali za shirikisho hilo.
Dereva la basi dogo la TFF (kulia), akisoma hati ya mahakama iliyotolewa kwa ajili ya kukamatwa kwa mali za TFF kutokana na deni la sh. milioni 51 linazodaiwa na Safina Holding.
Hati ya mahakama.
Sasa tunafunga na kuondoka nalo.
Wafanyakazi wa Jay Ambe Break Dowan wakichakalika na ufungaji wa basi la TFF tayari kwa ajili ya kuondoka nalo kutokana na deni wanalodaiwa na Safina Holding.
Gari dogo aina ya Toyota Crown lenye namba T 643 BJW likiwa limezuia gari la Jay Ambe Break Down lisitoke katika lango kuu la kutoka na kuingia katika Ofisi za TFF, baada ya mali za shirikisho hilo kukamatwa na dalali wa mahakama.
Hati ya kukamata mali za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ikiwa imebandikwa katika basi kubwa aina ya Youtong kwa ajili ya utekelezaji
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah akizungumza na waandishi wa habari wakati wa sakata hilo.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) leo wamejikuta wakipata aibu ya mwaka baada ya Kampuni yaFlamingo Auction Mart, kuyapiga tanganyika jeki mabasi ya shirikisho hilo kutokana na deni la zaidi ya
Sh.50 milioni la Kampuni ya Safina Holding ya jijini Dar es Saalam.
Kampuni hiyo ya Flamingo leo ilitia timu kwenye ofisi za shirikisho hilo kufuatia amri ya Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni ikitaka zoezi la ukamataji magari hayo hadi Juni 30 liwe limeshakamilika.
Fedha hizo za Safina Holding zimetokana na hifadhi ya baadhi ya timu zilizoshiriki michuano ya Kombe
la Kagame mwaka jana na Yanga kuibuka kidedea.
Magari ambayo yameamriwa na mahakama hiyo kukamatwa ni basi aina ya Yutong lenye namba za usajili T 581 CGR pamoja na Toyota Mini Bus lenye namba za usajili T 528 ASJ.
Lakini tofauti na amri hiyo ya Mahakama maofisa hao wa Flamingo walijikuta kwenye wakati mgumu
baada ya kuingia kwenye mzozo na maofisa wa TFF na kuzuka zogo kubwa huku maofisa hao wa TFF
wakiongozwa na Katibu mkuu Angetile Osiah kuzuia magari hayo yasichukuliwe.
Maofisa hao wa Flamingo wakiongozwa na Meneja Operation wao Noel Nyalila walitinga kwenye ofisi
hizo na kulifunga gari lenye namba za usajili T 528 ASJ aina ya Coster na kulivuta kwenye gari lao lenye
namba T 972 ABJ Jay Ambe, lakini walishindwa kuondoka nalo baada Osiah kuwaogoza wafanyakazi
wake kuzuia kwenye geti.
Wafanyakazi hao wa TFF waliamua kuzuia kwa kuegesha magari yao binafsi yenye namba T 643 BJW na
lingine lenye namba T 507 BER, hivyo kuzuia magari yaliyoamriwa kuchukuliwa.
Akizungumza kwa hasira Osiah alisema wamelazimika kuzuia magari yao kuchukuliwa kutokana na
utata wa tarehe iliyioandikwa kwenye amri hiyo ya Mahakama, ambayo alidai kuwa inaonyesha kwamba
inapaswa kutekelezwa Juni 31 mwaka huu.
“ Tumelazimika kuzuia kwa sababu mwanasheria wetu amekwenda mahakamani ili kupata udhibitisho
wa amri hii, kwa sababu tarehe ya kukamata magari haya ambayo ni Coster yenye namba T 528 ASJ na
basi lenye namba T 581 CGR ni kweli tunadaiwa lakini tuna mpango wa kulipa,” alisema Osiah.
Kwa upande wake Meneja Noel alisisitiza kwamba amri hiyo ni halali na wamefika hapo ili kuitekeleza
kwa kuwa hukumu ilitolewa April 23 mwaka huu, amri ikaandikwa Juni 3 mwaka huu, ambapo June 31
wanapaswa kurejea mahakamani. Hata hivyo waliomba msaaa wa Polisi ili waweze kusimamia
kuyachukua magari hayo.
No comments:
Post a Comment